SUNDAY CELEBRATION NA G.W.T NDANI YA VICTORIA SERVICE STATION LEO HII

Hatimaye baada ya kumaliza Jumapili ya Pasaka, sasa Glorious Worship Team wamerudi tena kukuletea mambo mema karibu yako, ambapo leo hii tena watakuwa ndani ya ukumbi wa Victoria Service Station kuabudisha na kulisifu Jina lake Yesu.

Pamoja nao watakuwepo walimu mbalimbali kwa ajili ya kufundisha vijana (na rika lote kwa ujumla) kuhusu mbinu za maisha. Wiki hii baadhi ya watakaohudumu ni pamoja na mwanamama Upendo Nkone, Mchungaji Emanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji), The Jordan Choir, Eric Shigongo na wengieo wengi.

Acha kufuata mkumbo, njoo upokee baraka zako bure bila kiingilio leo kuanzia saa tisa mchana hadi saa moja jioni. Kwani utakuwa na ratiba gani? Zifuatazo ni baadhi ya picha za kilichojiri wiki iliyopita, yaani Jumapili ya pasaka. Tukutane Victoria Servie Station kuanzia saa tisa alasiri. Ubarikiwe na BWANA Yesu!


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.