UKIZIMIA SIKU YA TAABU YAKO NGUVU ZAKO NI CHACHE

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.
Kila mtu kwenye maisha hupitia nyakati mbali mbali ambazo huwa ngumu na rahisi lakini kila mtu kwa wakati wake hufanikiwa kuvuka nyakati hizo ngumu akiwa salama na muda mwingine huanguka hata kwa nyakati zinazoonekana kana kwamba ni rahisi.

Taabu maana yake ni changamoto ngumu,tatizo gumu,nyakati mbali mbali ngumu.Katika kupita taabu mbali mbali za kimaisha cha kushangaza wengine wanavuka salama tena kwa urahisi lakini wengine wanashindwa kila nyakati ngumu wanazokutana nazo maishani mwao.Je Hawa wanaoshinda wanafanyaje na hawa wanaoshindwa wanafanyaje? Mara nyingi taabu nyingi tunazokutana nazo tatizo sio taabu mara zote nguvu za kutatulia taabu ndio tatizo kwa maana nyingine Mara zote huwa tatizo si tatizo .tatizo ni nguvu za kutatulia tatizo lililojitokeza wakati husika.

Je wengine wanafanyeje wakati wanapitia changamoto ngumu mapaka wanashinda? Ukifwatila Changamoto nyingi kwenye maisha zinajirudia ,hakuna changamoto mpya kwenye maisha yetu kama wanadamau.Unapoona kwako lilitokea basi kuna wakati lilishamtokea mwingine kabla ya wewe kukutokea.


1.HAUWEZI KUTATUA CHANGAMOTO UZUOPITIA KWA KIWANGO KILE KILE CHA AKILI KILA SIKU.

Hakikisha unaongeza kiwango cha akili katika kutatua changamoto zako za kila siku ndipo utakapouona ushindi wa kila eneo lako la maisha.Mara nyingi tunafikiria kwamba Changamoto zetu nig ngumu kumbe changamoto zote huanza na akili yako.Ukisema ni Ngumu basi akili yako itasema vivyo hivyo.Hakikisha unapngeza ujuzi na maarifa kwenye kutatua changamoto unazopiti.Ukitaka kupanda mlima Kilimanjaro  vyema na ukashindwa,tatizo sio kwamba Mlima Kilimanjaro umebadilika tatizo ni dhana unazotumia kupandia Mlima Kilimanjaro ndio sio sahihi.

2.ONGEZA KIWANGO CHA HABARI MAISHANI MWAKO.

Kizazi tunachoishi ni tofauti na vizazi vingine vilivyopita kizazi hiki ii kuishi napaswa kutumia akili nyingi kuliko nguvu.Ili kuongeza ufanisi katika utatuzi wa changamoto zako inakupasa uwe unafahaa vitu kadha wa kadha,Hakikisha unasoma kila mara vitu mbali mbali ambavyo unajua vinaweza kukuongezea thamani na Ubora katika Serekali ya Kichwa chako ndipo utakapoweza kutatua changamoto nyingi kwa urahisi na bila kutumia nguvu nyingi bila sababu za Msingi.Kizazi tunachoishi ni kizazi ch habari na maelezo kizazi kilichopita kilikuwa ni kizazi cha viwanda.Nguvu ilihitajika kwa wingi badala ya Habari na maelezo lakini kizazi hiki unapaswa kuwa na habari na maelezo mengi ili uweze kufanikiwa kwa urahisi zaidi.

3. JIFUNZE KUSIKILIZA WENGINE BILA MABISHANO NA MALUMBANO.

Unapojenga  namna rahisi ya kuwasikiliza wengine unajenga uwanda mpana wa kuweza kujifunza na kuongeza ujuzi wa kutatua na kupambana na changamoto unazokutana nazo.Mara nyingi tunapowasikiliza wengine huwa tunawasikiliza ili kuwajibu badala ya kuwasikiliza kwa lengo la kijifunza.Kumjibu mtu iwe ni hatua na mwisho juu ya kila anachokuelekeza au unachojifunza kwa lengo la kujifunza.Inawezekana kile unachopitia wewe sasa kwa kamsikiliza mwingine unaweza kupata na kujua suluhisho la namna ya kututua changamoto na tatizo unalopitia kwa sasa.

4. HAKIKISHA UNAKUWA NA MUDA WAKO BINAFSI WA KUTAFAKARI.

Mara nyingi tunapopitia nyakati ngumu ni watu wachache sana wanakaa chini na kutafakari kwa kina juu ya kile kinachowapa sasa na kufanya maamuzi yaliyo sahihi.Muda mwingi tunapopatwa na taabu na nyakati ngumu huwa tunafikia kufanya maamuzi badala ya kutuliza akili zetu kwa ukimiya na kiasi ili kuweza kushungulia swala linalotukabili kwa uhakika zaidi.Mara nyingi masuluhisho yetu huwa ya muda kwa sababu ya namna tunavyotatua changamoto zetu.Masuluhisho mengi yanakuwa ni ya kukurupuka yasiojawa na akili na utulivu matokeo yake baada ya muda ufakiri uliishinda taabu yako kumbe ndio kama umejipalia makaa ya moto.

Mwisho ,Ukiona unazimia siku ya taabu yako Tatizo Mara Nyingi huwa sio taabu inayokukabili bali nguvu zako ndio chache. Kuna aina nyingi za nguvu za namna ya kushughulika tatizo lako na taabu yako. Hakikisha unajenga misuli ya nguvu zako ili taabu ikija usizimie bali usonge mbele kwa ushindi mkubwa zaidi.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.