VIJANA WASHAURIWA KUPAMBANA NA NYAKATI ZA UJANA WAO

Engineer Carlos Mkundi
Mwimbaji maarufu nchini ambaye pia ni mkurugeni wa Upendo kwa Mama Foundation iliyopo jijini Arusha, Engineer Carlos Mkundi, amewataka vijana kujitahidi kupambana na maisha kwa sasa wakiwa na nguvu kabla uzee haujawakaribia.

Engineer Mkundi ameyasema hayo kutokana na kuwa na ongezeko kubwa la vijana ambao hawana ajira licha ya kuwa na elimu ya kutosha kuajiriwa na huku wengine wakichezea kazi.

Amesema kuwa licha ya serikali kupambana kila kukicha kuhakikisha vijana wanapata ajira na kupunguza idadi ya wasiokuwa na ajira bado kunachangamoto nyingi kwa vijana walio wengi kutokana na kuchezea kazi na wengine kutokutaka kujishughulisha na kuwa tegemezi katika jamii.

Engineer Mkundi amedai kuwa uzee haumruhusu mtu yeyote kufanya kazi kwa bidii jambo ambalo linafanya familia nyingi kuzidi kuwa masikini.

Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vya kiujasiriamali ili waweze kupewa mikopo kwa urahisi pamoja na kuhudhuria semina mbalimabli ili kuongeza ufanisi na nidhamu ya matumizi ya fedha.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.