AMENIFUTA MACHOZI YAKE EDNA KUJA KUZINDULIWA KESHOYakiwa yamebakia masaa machache kuelekea uzinduzi wa DVD ya Edna Kuja, hatimaye imefahamika kuwa maandalizi yote yako sawa sawa.

GK imemtafuta Edna ambaye ameelezea kwa kinaubaga namna ambayo mambo yatakuwa.


GK: Hii ni albam yako ya ngapi?

Edna: Ni albam ya pilli inaitwa pumziko la moyo

GK: Albam ina nyimbo ngapi?

Edna: Ina nyimbo sita

GK: kunatofauti gani kati ya albam yako ya kwanza na hii?

Edna: Duhhh tofauti zipo nyingi mpaka ujumbe

GK: Edna Kuja ni mtu wa namna gani? Kusifu zaidi ama kuabudu zaidi?

Edna: Zamani nlikuwa mtu wa kusifu zaidi na vile napenda kucheza ila sasa sijui ni kukua huku najiona nimekuwa wa kuabudu zaidi.

GK: Kwa nini mtu aache shughuli zake aje kujishughulisha kwenye tukio lako.Nini cha ziada?

Edna: Mungu atafuta machozi ya wengi na kubadilisha historia ya maisha yetu.

GK: Amen!

Edna : Oooh Yesu

Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.