HABARI PICHA: MAANDALIZI SACRIFICE OF PRAISE BARABARA, TUKIO JUMAPILI MCHANA

Sacrifice of Praise ni maono ambayo yalipatikana kutoka kwa kijana Dezzy Derick akiwa ndani ya ibada ambapo alionyeshwa kwamba licha ya kutakiwa  kumsifu Mungu, yatupasa pia kumpa Mungu dhabihu za sifa, ambapo kwa sasa Sacrifice Of Praise iko Tanzania, lakini ikiwa na malengo ya kufika hadi Sacrifice Of Praise Africa  

Katika maandalizi ya Sacrifice Of Praise Msimu wa pili jijini Tanga, mazoezi yamefanyika ambayo yamewashirikisha wahudumu mbalimbali ikiwemo Hellen Kijazi, Paul Clement, Christina Mesengu, Frank Chagoha, Angel Benard, Celestina Nyangusi, Shela Mnyanyi, Hope Singers, Mwang’ombe, Edna Kuja, Mise Anael  na wengine wengi ambao kesho wimbi la sifa litashuka Tanga.

Sacrifice of Praise Season 2 (msimu wa pili) kwa mara ya kwanza inafanyika katika mji wa Kiislamu, na watu wamejiandaa viliyo kutoa dhabihu za sifa. GK ambayo imepiga kambi Tanga kwa ajili ya kukuletea tukio hili, imeshuhudia wakazi wa jiji la Tanga wakiwa wamejiaanda vilivyo kupokea mawimbi ya sifa na kuabudu wa kuna mapokeo mazuri katika tamasha hili.

Tukutane E.A.G.T Mikanjuni saa nane kamili mchana.


 Edna Kuja katika maandalizi ya kesho
 Musiki nao ukiwa katika mpangilio wakeShare on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.