HAPPY BIRTHDAY TO OUR OWN AMBWENE MWAMWAJA

back in time...
Saa na siku zimepita, na hata majira tofauti yaja na kuondoka. Lakini ukuu wa Mungu tunaendelea kuushuhudia ndani yako kijana. Ni juzijuzi tu hapo mitaa ya Azania ulikuwepo - na sasa umesonga hatua nyingine.

Tunajivunia wewe kuwa sehemu ya Team GK, na hata sababu pia. Cha umuhimu kati ya yote ni kuendelea kumshika Mungu kwa hali na mali naye akapate kuzitimiza ahadi zake kwako maradufu.

Jumbe kutoka kwa fellow bachelaz WAPO.

"Shemejiiiiiii, nakutakia maisha marefu na yenye kumpendeza Mungu, zaidi Mungu akubariki na nikutakie kila la heri katika siku yako ya kuzaliwa." David Gile

"Ambwene Miachel ninakutakia maisha marefu na yenye baraka tele, na nipo katika maombi ya kufunga siku saba kuhakikisha mwaka huu haupiti bila Mungu kutenda muujiza kwa kutupatia shemeji, Mungu akubariki." Wilfred Nelson

"Sijui hata nasema nini... hebu angalia hizo picha hapo juu kwa makini, nadhani unaona tofauti yake. Kamwe usimuache Mungu - na bado safari inaendelea. Angalia usipotelee mwishoni." Silas Mbise

"Mweke Mungu mbele nawe utafanikiwa katika maisha yako yote." Costantino Pius

"Mi sina mengi sana, ila natumai unajua ulipotoka na hadi sasa Mungu alipokufikisha. Muheshimu naye akuheshimu maradufu." Elie John the Phiolosopher.

Hilo pilau likawe uwekezaji katika pilau kuu...

NB: By the way, kuna watu eti wanasema enzi hizo hata tai ulikuwa hujui kuiweka vizuri... :D
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.