HIVI PUNDE: JESHI BURUNDI LATANGAZA KUMPINDUA RAIS NKURUNZIZA

Baadhi ya waandamanaji leo Jumatano. ©AFP
Ikiwa na siku ambayo wakuu wa mataifa ya Afrika Mashariki wanakutana jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ajili ya kufikia muafaka kuhusu hatma ya aidha kugombea ama kutogombea kwa Rais Nkurunziza, Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza kuwa maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Burundi wamempindua Rais huyo.


Taarifa za awali zimemnukuu Meja Jenerali Niyombare akisema kwamba taifa hilo kwa sasa litaongozwa na Kamati ya Taifa ya Ukombozi (National Salvation Committee).

Wasaidizi wa Rais Nkurunziza ambaye yuko jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo na viongozi wenza wa Afrika Mashariki, Afrika Kusini na Marekani, wameelezea tukio hilo kama utani tu (upuzi).

Machafuko nchini Burundi yameanza mnamo tarehe 26 Aprili mara baada ya chama tawala nchini humo, CNDDFDD kutangaza kuwa Pierre atagombea kwa awamu nyingine, hatua ambayo mahakama ya kikatiba nchini humo iliidhinisha, licha ya kuwepo upinzani kutoka kwa baadhi ya wananchi, wakidai kwamba awamu zake mbili zinatosha, awamu ya kwanza ikiwa amechaguliwa na bunge la nchi hiyo mwaka 2005.

Mnamo Februari 2015, Rais Nkurunziza alimfuta kazi Meja Jenerali Niyombare kama mkuu wa ujasusi

"Kutokana na kiburi chake kutoheshimu jumuiya za kimataifa ambazo zimemtaka aiheshimu katiba na mkataba wa amani wa Arusha, kamati ya taifa ya amani imeamua, Rais Nkurunziza si kiongozi tena." Amenukuliwa Meja Jenerali huyo.

Tanzania imeshapokea zaidi ya wakimbizi elfu kumi kutokana na hali ya sintofahamu nchini humo, ambapo zaidi ya watu 20 wamefariki dunia kutokana na ghasia zilizoibuka kufuatia azma ya kugombea kwa awamu nyingine kwa Rais huyo.

Taarifa ya ziada kutoka Al-Jazeera na BBC

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.