KWA TAARIFA YAKO: BAADA YA MIAKA 10 YA NDOA MUNGU AMPA MTOTO NABII TANZANIA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.

Baba na Mama Amaris
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo nyumbani Tanzania, msomaji tumewahi kukushirikisha ushuhuda mkubwa wa baraka ambao Mungu aliutenda kwa mmoja wa maaskofu watiifu mbele za Mungu kutoka kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) pale Mito ya baraka Kariakoo, namzungumzia Askofu Bruno Mwakibolwa ambaye Mungu alitimiza kiu ya Askofu huyo ya kuwa na mtoto baada ya miaka 21 ya ndoa huku wengine walikuwa walishakata tamaa kuona askofu Mwakibolwa kuwa na mtoto wake wa kuzaa. Kama hukusoma BONYEZA HAPA.

KWA TAARIFA YAKO hata hivyo leo hatuko kwa Askofu Mwakibolwa ila tulikukumbusha tu, leo ni ushuhuda mwingine kutoka kwa Askofu na nabii Suguye wa kanisa la The Word of Reconciliation Ministries ambaye huduma yake ya kumtangaza Mungu inazidi kushamiri maeneo ya Kitunda jijini Dar es salaam. Kikubwa ni kwamba nayeye baada ya kusubiri kwa muda baraza zake kutoka kwa Mungu hatimaye mwaka huu Mungu amemjibu sawasawa na imani yake.

Sehemu ya waumini wakifurahia tukio hilo katika siku ambayo waliipa jina la Amaris 'Day'

Mke wangu nakupenda yani (ni kama vile Baba Amaris anamuambia Mama Amaris)

KWA TAARIFA YAKO Nabii Suguye ambaye awali kabla ya kuanza huduma yake rasmi alikuwa mwanakwaya wa kwaya ya Mwananyamala Evangelical Singers (MES) ya kanisa la Pentekoste lililopo Mwananyamala jijini Dar es salaam. Ni kwamba jumapili iliyopita alipata nafasi ya kumshukuru Mungu pamoja na mamia ya waumini wa kanisa lake na wageni mbalimbali katika ibada iliyofanyika kanisa analoliongoza maeneno hayo ya Kitunda akimshukuru Mungu pamoja na mkewe kwa kujaliwa baraka ya mtoto ambaye walimsubiri kwa hamu katika miaka 10 ya ndoa yao.

KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa Nabii Suguye ambaye huwa pia hurusha vipindi vyake kituo cha WAPO Radio FM iliyopo Kurasini jijini humo, amesema katika miaka 10 ya ndoa yake na mkewe wamewahi kupata mtoto ambaye hata hivyo alifariki na kwamba katika maombi yao kwa Mungu ambaye katika majibu yake kwao ni kwamba angewabariki kwa baraka hiyo mpaka pale ambapo wangemaliza kazi ya ujenzi wa kanisa analoliongoza nabii huyo jambo ambalo limetekelezwa na watumishi hao kwa kufanikisha sehemu kubwa ya ujenzi wa kanisa hilo.

KWA TAARIFA YAKO nabii Suguye na mkewe Mchungaji Anna Suguye wamesema katika kipindi chote hicho cha kutokuwa na mtoto waliona watu wakijikwaa kwa kuwasema vibaya huku wengine wakiwashangaa watumishi hao kutokuwa na mtoto wakati wapo mstari wa mbele katika kuwaombea wengine wapate watoto ambao Mungu alitenda kwa kuwafungua na kupata watoto lakini kwao ilikuwa bilabila. Lakini ni kwamba wakati wa Mungu haukufika bado na sasa amewabariki mtoto waliyempa jina la Amaris lenye maana ya ahadi ya Mungu na kwamba sherehe kubwa ya kumkaribisha mtoto huyo ilifanyika siku ya jumapili iliyopita.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kama nawewe unapitia hali ya kutokuwa na mtoto, GK inakwambia usivunjike moyo wala kukata tamaa endelea kuwa mwaminifu na mwenye subira kwa Mungu maana hujibu kwa wakati wake... Vinginevyo tukutane wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.