KWA TAARIFA YAKO JENGO LA KANISA LILILOUNGUA MARA MBILI, KWAYA YAKE HAISHIKIKI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Sehemu ya ndani ya kanisa la The Brooklyn Tabernacle.

KWA TAARIFA YAKO siku ya leo tupo nchini Marekani ndani ya jiji la New York katika kitongoji ama mji wa Brooklyn ambako tunakutana na kanisa la The Brooklyn Tabernacle linaloongozwa na mchungaji Jim Cymbala huku mkewe Carol Cymbala ndiye muongozaji mkuu wa uimbaji wa kwaya bora kabisa duniani ya The Brooklyn Tabernacle Choir ambao licha ya kupata tuzo mbalimbali zaidi ya tano kutoka Grammy na Dove awards pia ndio ilikuwa kwaya mahususi katika kuimba wakati Rais Barack Obama alipokuwa akiapishwa kuingia ikulu kwa awamu ya pili.


KWA TAARIFA YAKO kanisa la The Brooklyn Tabernacle (BT), ni kanisa ambalo linajumuisha waumini kutoka madhehebu mbalimbali ya Kikristo, limekuwepo mjini humo zaidi ya miaka 40 sasa likiwa na waumini zaidi ya 16,000 ambao hushiriki ibada kila wiki kanisani hapo. BT lilianza kwa kupitia misukosuko mbalimbali ambapo kwa mara ya kwanza mwaka 1847 likijulikana kama Central Presbyterian church wakitumia mali ya kanisa la kwanza la Presbyterian lililokuwa katika kona ya mtaa wa Willoughby na Pearl. KWA TAARIFA YAKO kanisa lao la kwanza ambalo lilikuwa pango la duka ama frame liliungua moto mwaka 1869 wakati huo wakipatikana katika kona ya mitaa ya State na Nevins.

Tazama video ya toleo lao jipya la 'Pray' wimbo At the Cross utunzi wake Freddy ambaye pia amenzisha wimbo huo


KWA TAARIFA YAKO kanisa la pili lilijengwa mnamo mwaka 1873 kwenye kona ya mitaa ya Marcy na Jefferson, ila kwa bahati mbaya kanisa liliharibiwa vibaya na kimbunga mwaka 1889. Kanisa la tatu walilijenga kwenye kona ya mitaa ya Clinton Avenue pamoja na Greene lilikiwa na uwezo wa kukalisha waumini 6000, kwa bahati mbaya liliharibiwa vibaya kwa moto mwaka 1894. Hata hivyo baada ya kuharibiwa na moto, uamuzi haukuwa kwa kanisa hilo kuhamia sehemu nyingine bali waliamua kujenga jengo lingine hapohapo.

Kanisa la The Brooklyn Tabernacle linavyoonekana kwa nje
KWA TAARIFA YAKO mchungaji kiongozi wa sasa Jim Cymbala na mkewe walianza utumishi rasmi katika kanisa hilo mwaka 1971 likiwa na waumini wapato 30 pekee ambao walikutana kwenye mitaa ya Antlantic Avenue mjini Brooklyn. Mnamo mwaka 1980 mambo yakaanza kwenda mbele baada ya kanisa hilo kufanikiwa kununua jengo la maonyesho lililokuwa likijulikana kama Carlton Theatre lililopo mtaa wa 292 Flatbush Avenue, 7th Avenue ambapo walilibadirisha jengo hilo kuwa katika muundo wa kanisa.

KWA TAARIFA YAKO baada ya kupitia misukosuko mingi yakiwemo ya kanisa lao kuungua, uongozi wa kanisa ukaamua kujitoa ndani ya dhehebu na kusimama lenyewe kwa kujumuisha waumini kutoka makanisa mbalimbali.

KWA TAARIFA YAKO kanisa hilo lilitoka katika jengo la Carlton na kuhamia katika jengo lililokuwa likifahamika kama Loew's Metropolitan Theatre lililopo mtaa wa Smith toka mwaka 2002 baada ya kulinunua jengo hilo na kufanyiwa ukarabati mkubwa ili kuwa na muonekano wa kanisa chini ya kampuni iliyofanya kazi hiyo ya Kostow Greenwood pamoja na Robert Silman ambapo marekebisho makubwa yaliyofanywa ni pamoja na kuhakikisha kwamba kanisa hilo linamuonekano wa kisasa katika kumuabudu Mungu na kuwa na vifaa vya kurekodia na muonekano. Ambapo kanisa hilo lina uwezo wa kukaa waumini walioketi 3,200 huku sehemu nyingine za jengo hilo zikifanywa kuwa ofisi, madarasa pamoja na ofisi za kutoa huduma za kijamii pamoja na vyakula.
Kwaya nzima ya The Brooklyn Tabernacle Choir wakiimba wakati wa kuapishwa Rais Barack Obama.

KWA TAARIFA YAKO kanisa hilo linaendesha ibada tatu kila jumapili, huku kwaya yake maarufu yenye jumla ya waimbaji 250 mpaka 300 ikiwa imejigwa mara mbili kwa wale waimbaji waanzishaji wa nyimbo na wachache wao kuwa ndio huwa wanatoka kwa mialiko ya mbali kwenye huduma (ila ukihitaji kwaya nzima bado pia watakuja) wakijulikana kama The Brooklyn Tabernacle singers, huku kundi lililobaki hutoa huduma kanisani hapo. Kwaya hii inajumla ya matoleo ya CD 29 toleo la 29 ambalo ni jipya limetoka mwezi uliopita likiwa limepewa jina la 'Pray' huku pia wakiwa na jumla ya matoleo matatu ya DVD. Licha ya kushiriki katika kuimba na waimbaji wengine maarufu, ndani ya kwaya hii kuna madaktari, wahandisi, watu waliponywa kutoka utumiaji madawa ya kulevya kama ujuavyo kanisa eneo lilipo kuna changamoto hiyo. Lakini pia kuna waimbaji ambao wamesomea muziki.


Baadhi ya waimbaji wa TBTC wakiimba wakati wa kuapishwa Rais Barack Obama
Baadhi ya waimbaji wa TBTC wakiimba wakati wa moja ya ibada kanisani kwao wakiongozwa na mwanakaka Freddy mbele ambaye pia yupo kwenye kiti cha Music director akishirikiana na mwanamama Carol Cymbala ambao ndio watunzi wakuu wa album mpya.
Video ya chini ni The Brooklyn Tabernacle singers (baadhi ya waimbaji kutoka kundi zima) wakiimba wimbo uliotungwa na Kirk Franklin katika moja ya huduma miaka iliyopita

Baadhi ya waimbaji wa TBTC wakiimba kwa hisia pamoja na mwalimu wao Carol Cymbala wakati wakirekodi toleo jipya la 'Pray' mwaka jana.Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo....vinginevyo tukutane wiki ijayo ]
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.