KWA TAARIFA YAKO: KAMA HUJUI KUHUSU UKRISTO DUBAI BASI HII INAKUHUSU

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Kanisa Katoliki la Dubai kama linavyoonekana bila msalaba nje©wikipedia

KWA TAARIFA YAKO hii leo nikukujulisha tu kama hulikuwa hulifahamu hili kwamba inapotajwa nchi za Falme za kiarabu (U.A.E) kitu ambacho kinawajia watu wengi akilini ni kwamba nchi hizo hakuna wakristo na kama wapo basi wanasali nyumbani kwao kwakuwa nchi hizo ni za kiislamu haiwezekani kuwepo kwa makanisa. Kama ulikuwa na mawazo kama hayo basi naomba GK leo ibadirishe fikra zako kidogo.


KWA TAARIFA YAKO leo tutakujulisha kuhusiana na mji maarufu ambao watanzania wengi hupenda kwenda kwa shughuli za kibiashara, nazungumzia Dubai, moja ya mji wenye sifa kemkem na matumizi ya gharama kabisa, ikiwemo magari ya kifahari ambayo kwa nchi nyingine huwezi kukuta askari polisi wakiendesha magari aina ya Lamborghini katika doria lakini kwa mji huo ni kitu cha kawaida. Sasa turudi kwenye taarifa husika, ni kwamba katika mji huo kuna zaidi ya makanisa 13 yanayofunguliwa na kuendesha shughuli zake za ibada kama kawaida, kumbuka serikali ya Dubai haitambui uhalali wa madhehebu ya Kikristo kisheria, lakini imewapa uhuru wa kuabudu wakristo.

Baadhi ya umati wa wakristo wakiwa kanisani jijini Dubai

KWA TAARIFA YAKO kati ya makanisa hayo ni pamoja na kanisa la Baptist, Katoliki,Anglican na makanisa mengine yakiwepo ya Kipentekoste ili kujionea moja ya idadi ya makanisa hayo na namna unavyoweza kuwasiliana nao BONYEZA HAPA. KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2005 imefahamika kwamba asilimia 76 katika mji wa Dubai ni Waislamu huku watu wa bara la Asia pamoja na dini zao wanakamata asilimia 15 mwisho kabisa ni Wakristo wenye asilimia 9 pekee kwa mujibu wa sensa hiyo. 

Wakristo wakijifunza Biblia jijini Dubai
KWA TAARIFA YAKO serikali ya Dubai imeruhusu kuwepo kwa dini nyingine kwa masharti yakiwemo ya makanisa kuto weka alama za msalaba nje ya nyumba za kuabudia wala kujenga minara ya kengele, huku wanaume wakikristo wakikatazwa ama kutoruhusiwa kuoa wanawake wakiislamu. Aidha mambo mengine ni pamoja na Wakristo kukatazwa kueneza injili ama Ukristo katikati ya Waislamu ama kuwa huru kuzungumza kama Tanzania. KWA TAARIFA YAKO mnamo mwaka 2007 mshauri wa Rais masuala ya kidini wa mji huo Al - Hashemi alihudhuria ibada ya Krismasi katika kanisa la Anglikana mjini humo. Takribani siku zinavyokwenda ndivyo Ukristo unavyozidi kukua katika nchi za Kiarabu Dubai ikiwa moja wapo.

Moja ya tukio la Kikristo jijini Dubai

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo, kikubwa ni kuzidi kuomba ili injili ikue zaidi na watu wamjue Mungu wa kweli. ……vinginevyo tukutane wiki ijayo...

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.