KWA TAARIFA YAKO: MWIMBAJI WA "SIONI MWINGINE WA KUMWABUDU" ALIVYOPEWA WIMBO KUPITIA SADAKAKati ya nyimbo ambazo kwa mwaka huu zimekaa akilini na mioyoni mwa watu, ni wimbo wa Sioni Mwingine tena. Wimbo huu ambao kuanzia vibandani wanapouza memory card hadi kwa mafundi simu. Licha ya kwamba wimbo nimarufu, wachache wanafahamu kwamba wimbo huo umetolewa mwaka 2011, na kwamba umeimbwa na mwanaume. Pamoja na kufahamika kuanzia mwishoni mwa mwaka 2014 na hata kuvuma zaidi kufikia 2015, Sioni Mwingine tena ni wimbo ambao umetungwa katika mazingira ya ajabu, kwani ni kwa namna ya kipekee, kutoka muimbaji kushushwa madhabahuni kwenye mass choir mbele ya umati wa kanisa, hadi kuwa kiongozi wa waimbaji.

 KWA TAARIFA YAKO siku ya tukio, Martin Murunga anaeleza kwamba alipanda madhabahuni pamoja na mass choir (yenye waimbaji kama 500) tayari kwa kuanza na ibada yakusifu na kuabudu, kabla kiongozi wa kwaya akamjia na kumtaka ashuke mara moja, “wewe ni nani hadi udhani unaweza kuimba” ndio maneno ambayo

KWA TAARIFA YAKO yalielekezwa kwake, ambapo hakuwa na budi kushuka huku aibu kuu imemshika. Pamoja na siku hiyo kuwa chungu sana, Martin Murunga hakukata tamaa, safari yake iliendelea kwa kujikongoja huku akimuanmini Mungu kwamba, ipo siku. Siku moja kukawa na waimbaji wageni kutoka Marekani, Napenda kile kiko ndani yenu, nasikia kupokea. Ni maneno yake kwa kundi hilo la uimbaji, na kisha kuwapatia shilingi elfu 7 za Kenya, ambazo ndizo zikawa mbegu katika huduma yake.

KWA TAARIFA YAKO hii ni sauti aliyoitii kutoka juu. Mwaka uliofuatia kwenye kongamano kubwa kama lile ambalo aliaibishwa mara ya mwisho, alitakiwa kuongoza sifa siku ya Jumamosi. Hapo ndipo akaomba Mungu ampe jambo la kuaibisha maaudi zake, na japo aliimba pambio la kawaida tu, mtu mmoja kutoka Afrika Kusini akapanda madhabahuni kutaka kupokea sehemu ya upako huo, na ndipo walipofuata wengine kummiminia pesa za kutosha, ambapo jumla alikusanya takribani milioni moja na nusu za Kitanzania.

 KWA TAARIFA YAKO pesa zote hizo alizitoa poa hapo kanisani, jambo ambali wengine walimshangaa, lakini sauti ya Mungu ilimueleza afanye hivyo. Kuitii sauti ya Mungu ndio kulimpa baraka zaidi. Aliendelea kumtumainia Mungu na hatimaye siku moja kuelekea mlimani kwa siku tatu, ambapo ndipo alipopewa wimbo huu. Sioni Mwingine Tena ikaendelea kusikika kichwani mwake. KWA TAARIFA YAKO aliposhuka, ndipo alipojitokeza binti mmoja na kumpatia milioni moja (thamani ya shilingi ya Tanzania) kwa ajili ya kurekodia. Kwa maelezo ya Martin, anasema kwamba kati ya kitu alichoomba ni Mungu kujitwalia utukufu kupitia wimbo huo, na si yeye kufahamika kwayo.


Na hiyo ndio KWA TAARIFA YAKO wimbo unafahamika zaidi ya yeye anavyofahamika, licha ya kwamba pia imempa changamoto ya kuibiwa, kwa baadhi ya watu wakijifanya ndiye yeye. Kufika kwake studio kuliwaduwaza waandaaji wa muziki, kwani hakuwa na karatasi aliyoandika wimbo huu, bali ulikuwa ukitokea kichwani, na pia aliwaeleza kwamba anataka kuimbia 'key ya D’ ambayo mara nyingi wakinadada hutumia. Pamoja na wasiwasi kutanda kwa ‘maproducer’ hao,


KWA TAARIFA YAKO alirekodi vema, na kati ya mambo ambayo yanamuwezesha kucheza na sauti ni kwa kuwa amesomea muziki. Usitake kwenda mbio, nenda na wakati wa Mungu,


KWA TAARIFA YAKO huo ndio ujumbe  anaowaachia waimbaji nchini. Akigusia kurekodi kwake 2011, hadi kuja kuenea kwa wimbo huo nchini mwaka 2015. Nyakati za wmisho zimefika, si kila muimbaji ameokoka, si kila muimbaji anamcha Mungu, wengine ni biashara, lakini kila kitu unachofanya, Mungu ndiye anajibu, na utajibu siku ya mwisho kama kweli ulikuwa unafanya kwa makusudi mazuri. Anamaliza kuieleza GK.


Hiyo ndo KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo.

Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.