MAKOSA TUNAYOYAFANYA KUHUSU AKILI ZETU

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.
 

MAKOSA TUNAYOYAFANYA KUHUSU AKILI ZETU.

1. UTEGEMEZI
Umekuwa ni utamaduni kwenye jamii zetu kwamba kuna watu wanasika sana kwenye maswala yanayohusu akili zetu.Jamii yetu ni watu wachache ambao huchukua muda kuboresha na kujifunza ili kuongeza akili zao.Akili ni jambo ambalo linakuwa na linapungua,hakuna mtu ambaye amepewa dhamana ya kuongeza a akili yako.Mara nyingi tumejenga utamaduni kuna watu ambao wana akili sana kuliko wengine na wao ndio wamepaswa kuwafundisha wengine wawe na akili kama wao. Hakuna mtu ambaye anahusika na ukuaaji wa akili yako,iwapo haukuwekeza muda wa kuikuza na kuiongeza akili yako maana yake itadumaa na inaweza kufikia kiwango cha chini kabisa.

2. MUDA
Kujifunza ni jambo ambalo lipo kila muda hakuna muda maalumu wa kusema hapa najifunza na pale sijifunzi.Mara nyingi tumekuwa na utamaduni kwamba kuna umri fulani unapaswa kujifunza na kuna umri haupaswi kujifunza ,jambo ambalo si lakweli.Maadamu unaishi imekupasa kujifunza kila siku bila ukomo.Akili ni jambo ambalo unalo siku zote si jambo ambalo linakuja na kuondoka , imekupasa kujifunza bila kikomo mpaka siku utakapondoko duniani.Siku ambapo utaacha kujifunza ndipo wakati ambapo unaweza ukawa umeanza kufa ,ni afadhali kufa kifo halisi kuliko kuanza kufa kwa akili.Maana kufa kwa akili kuna athari kubwa zaidi kuliko kufa kwa mwili.Mara nyingi dunia ya tatu hatupendi kuwekea muda mwingi kwenye akili zetu.

3. UKOMO
Hakuna ukomo wa kujifunza,kujifunza ni jambo endelevu unapoweka ukomo wa kujifunza maana yake unakuwa na akili iliyoduma,akili nii jambo linalokuwa na kuongeza .Akili ni mithili ya shamba la ngano .Shamba la ngano haliwekewi ukomo mpaka mavuno yatakapofikiwa.Siku ambapo utasema niache hapa kupalilia shamba lako ndipo siku ambapo magugu yataota.Akili isiyopaliliwa kila siku ambayo imewekewa ukomo,ni akili ambayo imejaa magugu na ni hatari pia kwa afya ya maisha ya kawaida.Akili ikishaanza kuathirika na magugu jambo linalofwata ni kifo halisi kwenye kila Nyanja na maendeleo yakiwepo ni duni.

4. AINA YA HABARI TUNAZOSOMA.
Ni muhimu kujua faida ya habari tunazosoma kila siku maana kuna wakati huwa tunapenda kusoma kila kitu ambapo muda mwingine ni sumu kwa akili zetu.Ni muhimu kuwa na chanzo sahihi cha kuweza kusoma habari ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina na zenye uhakika.Unapoaanza kujifunza kila siku imekupasa kuweka mihemuko pembeni.Maana ukiweka mihemko mbele unaweza usijue kipi ni chakula bora kwa afya ya akili zako.Habari unazosoma,unazoona, unazosikiliza kila siku ni chakula katika akili.Iwapo chakula kikiwa na sumu basi hali kadhali akili inaweza kufa na kupotea kabisa.Ni muhimu kuweka mipaka kwa habari unazoona sio za lazima kuzisoma na ni hatari kwa afya ya akili yako.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All.

    Share on Google Plus

    About Ambwene Mwamwaja

    This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.