MASWALI MATANO YANAYOWEZA KUKUSAIDIA KUJUA KAMA UNAISHI MAISHA CHANYA/HASI


Na Faraja Naftal Mndeme, 
GK Contributor.

MASWALI MATANO YANAYOWEZA KUKUSAIDIA KUJUA KAMA UNAISHI MAISHA CHANYA/HASI. 1. JE HUWA UNAPENDA KUONGELEA HABARI ZA WATU WENGINE KWA NAMNA GANI? Ujenzi wa tabia njema ni swala linalochukua muda na si jambo ambalo ni la ghafla linaloweza kujitokeza tu kama upepo wa kisuli suli.Mara nyingi tumekuwa na tabia za kila namna bila kujua namna zinavyoweza kuathiri maisha yetu ya kila siku.Je umeshawahi kukutana na mtu unamwuliza kitu kuhusu mtu mwingine habari ya kwanza anayoanza kukuambia ni ubaya wa mtu? Je unapoeleza ubaya wa mwingine inakusaidia nini? Je unapoongelea ubaya wa mwingine kuna thamani gani unayoweza kuongeza kwenye maisha yako ya kila siku? Je kama umeweza kuelezea ubaya wa mwingine mbele ya mtu fulani ,je ni kipi kinakushinda kwenda kuelezea ubaya wa huyo unayeongea naye kwa mtu mwingine? Ukitaka kujua iwapo unaishi maisha chanya/hasi angalia namna unavyomwelezea mtu mwingine kwa watu wengine.Ni muhimu kujua kwamba kipimo unachotumia kuelezea ubaya wa mwingine hakipo ndani ya mtu mwingine kipo ndani mwako unaweza ukajikuta unajielezea wewe mwenyewe bila kujijua namna ulivyo ndani.Hakikisha unajifunza kuwaelezea wengine vyema bila kujali namna walivyo. 2. JE UNAPENDA KUSIKILIZA HABARI MBAYA ZA WATU WENGINE? Muda mwingine huwa tunaingiza magonjwa na sumu kwenye akili zetu bila kujua.Akili huchukua kila jambo linalokuja mbele yako,ni muhimu kujifunza namna unavyokusanya habari na kuziiingiza kwenye akili zako.Akili inayokusanya habari mbaya za watu wengine huendelea kuchakata habari mbaya ndani kwa ndani na mwisho wa siku Unapotaka akili itoe kitu chema inakuwa ngumu maana mali ghafi unazoingiza ndani ya akili zako ni sumu na takataka.Akili ni mfano wa Shamba ,Hauwezi kuliachia shamba likaota majani alafu ukategemea siku moja utavuna mpunga.Unapotarajia kuvuna mpunga hakikisha unapanda mpunga.Mara nyingi tumeshindwa kufahamu kwanini akili zetu huwa hazifanyi kazi kwa kiwango cha juu kama watu wengine.Kumbe maisha yetu ya kila siku ndio yanayoleta uharibifu kwenye akili zetu bila wewe mwenyewe kujijua.Iwapo unapenda kusikiliza habari njema za watu wengine zitakujenga na kukuinua na kukupa kukusaidia kuongeza upeo wa akili lakini unapopenda kusikiliza mabaya ya watu wengine tambua unajiharibu mwenyewe. 3. JE UNAWAHUKUMU WENGINE KUTOKANA NA YALE UNAYOYASIKIA? Watu dhaifu wa fikra hujenga hukumu kwa watu wengine bila kuwa na ushahidi wa kina bali watu wenye nguvu huepika kuhukumu sababu wanatambua kwamba wanayo nafasi ya kujifunza kutoka kwenye makosa ya watu wengine. Katika jukwaa la Kisheria kuna jambo linaitwa Sheria ya Ushahidi.Sheria ya Ushahidi ni swala ambalo Mahakama haiwezi kutoa hukumu kwa namna ya kusikia tu.Mahakama hutoa hukumu kwa namna inavyopata ushahidi wa kutosha kutoka kwenye maeneo mbali mbali na wenye tija.Mara nyingi maisha yetu ya kila siku katika jamii zetu tunaendesha kwa kuamini magazeti ya udaku na magazeti tunayoyaita ni pendwa tunasahau magazeti hayo hutafuta fedha bila kujali athari za kisaikolojia kwa wasomaji.Ni Muhimu kuhakikisha kabla jambo lolote hujalifanyia hukumu unakuwa na ushahidi wa kutosha na kama unaona huwezi kuupata ushahidi wa kutosha ni muhimu kuhakikisha unatumia muda wako kujijenga na kujiendeleza katika Nyanja mbali mbali.Kipimo kile kile unachokumu wengine ndicho na wewe utakuja kuhukumiwa siku moja.Ili kuepuka kuhukumiwa basi acha kuhukumu wengine pasipo na ulazima. 4 . JE UNAWEZA KUTUNZA SIRI ZA WATU WENGINE ? Muda mwingi tumewaumiza wengine kwa namna vile walivyotuamini na kutueleza mambo yao ya siri na huku wakitutaka msaada lakini matokeo yake tumegeuka na kuwa watangazaji wa siri za watu hao kwa watu wengine bila kujua athari zake kwetu sisi binafsi.Katika kizazi hiki cha mitaandao ya kijamii imekuwa ni rahisi mtu kueleza siri za mtu mwingine bila kujali.Lakini tuaangali upande wa pili kama umeweza kueleza siri za mwingine je siku utakapokuwa na shida je ni kipi kinakuuzuia kuweka siri zako hadharani? Tabia ni swala linalojengeka muda mrefu tena kwa utaratibu.Tabia inaweza kujengwa moja kwa moja na muhusika lakini pia inaweza kujijenga yenyewe bila muhusika kujua na matokeo yake siku inapoaanza kuonyesha athari zake mtu anaweza asigundue na anaweza kuona yupo sawa sababu ni kitu ambacho kipo ndani mwake.Watu walioko nje ndio wanaweza kufahamu kwamba hapa kuna tatizo na matokeo yake wataanza kukukimbia maana watajua wakikkueleza mambo yao siku watayakuta hadharani bila wao kujua.Unapoeleza siri za watu wengine si kwamba unawaathiri wao ila unajiaathiri wewe mwenyewe bila kujijua. 5. JE UNAPOELEZA MAKOSA YA WENGINE NDANI MWAKO UNAJISIKIAJE? Moja ya kipimo kimoja ni vile unavyojisikia ndani mwako unapoolezea makosa ya mtu mwingine,je inakupa furaha au inakupa huzuni.Ukiona unajisikia furaha kuelezea makosa ya mtu mwingine basi tambua maisha unayoishi ni hasi na inakupasa ubadilike haraka la sivyi kuna wakati utaanza kushuhudia athari zake kwenye maisha yako kwa namna isiyo ya moja kwa moja.Ni muhimu kujenga taswira njema unapoeleza makosa ya watu wengine.Mokasa ya watu wengine ni sehemu ya shule moja wapo ambayo tunaweza kuipata na kutongezea ujuzi wa namna tunavyoweza kuishi hapa duniani. Unawezausione athari za moja kwa moja kwa ile furaha unayoipata kwa kuelezea mabaya ya watu wengine baada ya muda fulani kupita unaweza kukuta akili yako umegandamana na tabia zile zile mbaya ulizokuwa unazizungumza mara kwa mara kwa wengine.Huwa tunasahau kwamba kile unachosikia muda mrefu ndicho kinachokaa ndani mwako.Ni muhimu kuhakikisha unaifuka tabia hii mbali na wewe kwa gharama yoyote ile. E-mail:naki1419@gmail.com +255788454585 God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.