MPUMBAVU MWENYE HEKIMANa Faraja Naftal Mndeme, 
GK Contributor.

Siku Mmoja mtu mmoja alijulikana ni kama Mpumbavu kwenye Mji wa Shinari huko Mashariki mwa nchi ya Babeli.Mtu huyo alipewa jina la Mpumbavu kwa sababu kila alishofanya kilionekana ni cha Kipumbavu wala hakuna aliyemtilia maanani kutokana na kiwango chake cha juu cha Upumbavu alichokuwa nacho. Siku Moja Mtu huyu aliyejulikana kama Mpumbavu aliamua kununua shamba kutoka kwa Mtu mwingine aliyejulikana kana kwamba ni mtu mwenye hekima kuliko watu wote katika Mji wa Shinari,Maana Mtu huyu aliheshimiwa sana na watu kutokana na uwezo wake wa hekima alizokuwa nao. Baada ya Muda kidogo kupita katika shughuli zake za kila siku huyu mtu aliyejulikana kana kwamba ni Mpumbavu aligunndua shamba alilonunua lilikuwa na kiasi kikubwa cha Dhahabu lakini aligundua kwamba Mji ule ulikuwa na Matajiri wengi na Wenye Hekima wengi iwapo watagundua kwamba shamba lake alilonunua kutoka kwa mwenye hekima atanyang’anywa na atadhuliwa. Kila siku jioni alikuwa akikaa chini ya mti wa shamba alilokuwa amenunua na lenye dhahabu akifikiria namna gani anaweza kuziuza dhahabu zake bila wale wenye Hekima na Matajiri Kugundua kwamba dhahabu hizo zinatoka shambana mwake. Baada ya Siku Nyingi kupita aliamua kuzichimba zile dhahabu na kuamua kwenda kwenye Mto Mkubwa wa Maji katika Mji Ule Wa Shinari na Kuamua kuzimwaga zile dhahabu kando kando wa wa Ule Mto,Kazi hiyo aliamua kuifanya usiku wa manane mpaka alfajiri alipomaliza kuifanya kazi ya kuzimwaga zile dhahabu akaenda zake kupumzika. Kulipokucha asubuhi yake akakuta kila mtu anazungumzia zile dhahabu na ndipo alipoamua kuwaambia wale watu wa mji kwa kutangaza Mbiu kwamba Dhahabu zile ni feki ,wale wenye hekima walipomsikia akipiga mbiu na akiwaonyesha kwamba yeye ndio aliyezitupa na akawapeleka kuwaonyesha mashimo aliyozichimba watu wa mji ule pamoja na wale wenye hekima na matajiri waliamini kwamba Dhahabu zile ni feki.Ndipo wale Matajiri na Wenye Hekima walijitoa kutoka kwenye mananunuzi ya dhahabu zile maana walishaambiwa ni feki na Yule Mtu aliyejulikana kama Mpumbavu kuliko wote katika mji ule. Basi Yule Mpumbavu akawaagiza watu wa mji ule kwamba yeye ananizinunua dhahabu feki kwa bei nzuri,yoyote aliyekuwa tayari aje amuuzie .Baada ya Masaa kadhaa watu walikuja kumuuzia dhahabu zile Yule Mpumbavu bila kuzipeleka kwa wataalamu wa kupima na wenye kuzijua dhababu na ndipo dhahabu zile zote zikarudi kwa Yule Mtu aliyejulikana kana kwamba ni Mpumbavu kuliko wote kwenye Mji Ule wa Shinari katika Nchi ya Babeli.Basi Mtu Yule aliyejulikana kana kwamba ni mpumbavu aliamua kwenda kuziuza dhahabu zile kwenye nchi ya Mbali na Mara aliporudi alionekana kana kwamba ni Mtu tajiri kuliko Matajiri wote Waliokuwako katika nchi ya Babeli na Mji Ule wa Shinari. Je Ni Nani aliyekuwa Mpumbavu Katika Mji Ule wa Shinari katika nchi ya Babeli? Je Umejifunza nini kutokana na mfano Huu? E-mail:naki1419@gmail.com +255788454585 God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.