MWIMBAJI JOYOUS CELEBRATION AMALIZA MKATABA NA KUMRITHISHA NAFASI YAKE MDOGO WAKE

Bheka Mthethwa kwenye gitaa la bass akiwa na kijana Lungelo kwenye kinanda.
Aliyekuwa mpigaji gitaa zito la bass wa kundi maarufu la Joyous Celebration la Afrika ya kusini Bheka Mthethwa ambaye amejiengua kutoka katika kundi hilo baada ya kumaliza mkataba wake ameamua kumrithisha mdogo wake wa damu aitwaye Qhubekani Mthethwa kushika nafasi yake ndani ya kundi hilo.
Bheka ambaye alianza rasmi kazi yake ndani ya Joyous kwa kurekodi toleo la 15 akiwa amechukua nafasi ya mkongwe mwingine aliyekuwamo kundini humo aitwaye Sabelo Masondo, alianza kukalia benchi wakati wa uzinduzi wa DVD ya 19 ya kundi hilo wakati wa pasaka mwaka huu, ambapo alikaa kwa watazamaji na kuonyesha furaha yake kuwaangalia Joyous wakiimba zaidi alimsifu mdogo wake kwa upigaji mzuri.

Aidha Bheka ambaye alianza kutayarishwa mapema kabla ya kuondoka kwa Sabelo alikuwa anapiga gitaa hilo katika shindano la 'I want to sing gospel' lililochini ya mmoja wa viongozi wa Joyous bwana Lindelani Mkhize ambapo baada ya kuondoka kwa Sabelo akaianza kazi hiyo rasmi. Mtindo huo wa wapigaji wa Joyous kuacha mtu wa kuziba mapengo yao mara watakapomaliza kazi yao umeanza kitambo ambapo, Nqubeko kabla hajaondoka unaweza kumuona katika DVD ya 16 ya Joyous alivyomwachia kiti Siyanqoba Mthethwa kuongoza jahazi kwa baadhi ya nyimbo katika DVD hiyo ambayo ilikuwa toleo la mwisho la Nqubeko ambaye pia aliachiwa kiti hicho na mchungaji Mthunzi Namba kiongozi wa Joyous.

Qhubekani Mthethwa mpigaji mpya gitaa la bass wa Joyous Celebration, kiwango kimempa ajira.
Mdogo wake Bheka alianza kujipenyeza katika Joyous 18 kupitia wimbo Mbongeni ambapo alikuwa anapiga gitaa la bass namba mbili wakati kaka yake akiongoza na bass namba moja. Aidha kijana huyo licha ya kwanza ndio ameianza rasmi kazi katika Joyous, bado atakuwa na uhuru wa kuonyesha kipaji chake hasa kutokana na kujiunga na rafiki zake wa siku nyingi akiwemo kijana Lungelo Mnqobo. Huku pia kazi yake aliyoifanya na kijana Khaya Mthethwa mshindi wa SA Idols na mwimbaji wa zamani wa Joyous kupitia album yake ya Uprising ni kipimo kingine cha kijana Qhubekani kuwa kipaji kimempa ajira ndani ya Joyous.

Katika watu waliorithishwa viti na kuonekana kupwaya ni mpigaji ngoma wa kundi hilo kijana mwenye asili ya Kinigeria Ire Bolaji ambaye licha ya kupewa kazi hajawahi kurekodi na kundi hilo na hata mwaka jana Siyabulela alipopata ajali hakuitwa kuziba nafasi yake katika kurekodi na badala yake aliitwa Bafana Sukwene kuziba nafasi hiyo.

Kwa upande wake Bheka amejizolea sifa kutokana na upigaji wake mahiri pamoja na kuwa mbunifu kwa kutumia gitaa hilo ambapo tayari alifanikiwa kuandaa maonyesho yake kwakuwa pia anasifika kwa kuimba sambamba na kurekodi wimbo na Joyous huku gitaa lake likiwa ndio linaongoza wimbo huo.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.