PICHA 250+ UZINDUZI WA DVD YA AMENIFUTA MACHOZI YA EDNA KUJA

Mgeni Rasmi, Dkt Furaha Mramba akiizundua rasmi DVD ya Mrs Edna Kuja
Jumapili ya kwanza ya mwezi Mei ilikuwa ya kipekee hasahasa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo walipata fursa ya kusheherekea pamoja na waimbaji wa Injili kwenye uzinduzi wa Amenifuta Machozi ya kwake Mrs. Edna Kuja - kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza.

Zaidi ya waimbaji 25 walikuwepo kuhakikisha kwamba Injili kwa njia ya uimbaji inafikishwa kwa mahadhi tofauti tofauti. Tukio hillo ambalo liliandaliwa na One Voice Family International, lilishuhudia waimbaji wa kila aina na kutoka mikoa mbalimbali nchini walisifu Jina la BWANA Yesu, huku mgeni rasmi, Dkt Furaha Mramba, ambaye ni Kaimu Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maabara Tanzania, Wizara ya Mifugo alisisitiza kwa waimbaji kujiweka sawa mbele za uso wa Mungu ili wapate kuunganisha watu sawa sawia na mapenzi ya Mungu.

Baadhi ya waimbaji waliokuwepo ni kama vile Jesca Emmanuel, Jessica BM, Loveness Mwaikaja kutoka Singida, Bomby Johnson, Miriam Mauki, Furaha Isaya, Betty Lucas, Upendo Kilahiro, Ester Shedafa, Lilian Kimola, Kinondoni Revival Choir, Christina Matai na Upendo Group, na wengineo wengi.

Tupitie picha kwa pamoja sasa.
Loveness Mwaikaja kutoka Singida (One Voice)MC Joshua Silemba, we muite Baba D  (One Voice)


MC Mkolosai the Boy. Serikalini anaitwa Emmanuel (One Voice)Ester Shedafa (One Voice)

Alfa Melody SDA
Mashuhuda

Eliezer Mang'wela kutoka Arusha (One Voice)

One Voice Family International wakisuburi kumpokea mgeni rasmi.

Mgeni Rasmi, Dkt Furaha Mramba akawasiliFuraha Isaya naye akabariki mamia ya watu waliofika (One Voice)Upendo Group
Ikafika zamu ya Veronica kutoka Morogoro (One Voice)Sasa tuelekee Mwanza kwake Betty Lucas (One Voice)


Kinondoni Revival Choir hawa hapa


Wakati huohuo, dakika chache kabla ya kuingia ukumbiniKinondoni wanaendelea
MC Baba D akatuletea rasmi Edna jukwaani.
Aliyekusanya watu hatimaye akapanda
Sasa ni zamu ya Risala
Loveness Mwaikaja akisoma risala kwa mgeni rasmi

Edna Kuja akakuja tena jukwaani

Mgeni rasmi akapanda kuzindua rasmi

Kisha akaachia upako wa dola


Standby

Wageni waalikwaHawa ni classmatesWith mom & dad
standby
 Upendo Kilahiro akapanda

'jamani hongeraa'


More than conquerorsTafakuriRehema Magembe akagusa mioyo Mr & Mrs
Tukafunga kwa maombi
 Kisha tathmini fupi na kikao cha familiaBwana Yesu awabariki kwa kufika jamani.

Ulifanikiwa kuwepo siku hiyo? Kama mvua haikuwa kikwazo, basi tuambie kwa mtazamo wako kwa uliyoyaona. GK tumemaliza kukuhabarisha kwa hili, ila vipande vya picha za sauti utavipata kupitia ukurasa wetu wa youtube.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.