PICHA YA MAHARUSI WAKIMUOMBA MUNGU KWA HISIA KABLA YA SHEREHE YAO YAWAGUSA WENGI

Caleb na Maggie wakiwa katika hali ya maombi


Picha ya maharusi wakimuomba Mungu kwa hisia kabla ya sherehe yao ya ndoa iliyosambaa mitandaoni huko nchini Marekani ikimuonyesha mfanyakazi wa kikosi cha majini Caleb Earwood na mkewe Maggie kutoka eneo la Asheville huko Kaskazini mwa Carolina nchini Marekani imetajwa kuwabariki wengi waliofanikiwa kuitazama.

Maharusi hao kwa pamoja walijiweka katika moja ya kona na kuanza kumuomba Mungu huku wakiwa wamezungukwa na marafiki zao kabla hawajaanza safari yao mpya ya mume na mke. Ambapo kwa mujibu wa taarifa maharusi hao wamekuwa marafiki toka wakiwa wanafunzi sekondari na kuanzisha uhusiano miaka miwili iliyopita. Bwana harusi Caleb (21) amesema walikuwa ndio waaanza kupiga hatua za mwanzo katika maisha ya ndoa pamoja, na kwamba hawakutaka kupiga hatua bila kumshirikisha Mungu, amesema alimuomba Mungu juu ya mkewe huyo mrembo na mwenye akili kwamba afanyike baraka sambamba na familia ya mkewe.

Kwa upande wa bibi harusi Maggie (22) yeye amesema anajisikia usalama kujua mtu anayeolewa naye anahisia sawa na zake kuhusu Mungu. Ambapo bwana harusi Caleb alisema wanashukuru kwamba picha yao waliyopigwa na mpigaji maalumu wa harusi yao bwana Dwayne Schmidt imeweza kubariki na kugusa mioyo wa wengi.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.