RAHISI NI GHARAMA, JE GHARAMA NI RAHISI?

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

Hakuna jambo lolote kwenye maisha ambalo linakosa gharama ,gharama ni jambo ambalo haliepukiki kwenye maisha,Unapoamua kuacha kugharamia kitu maana yake kitu hicho hakina umuhimu na thamani kwenye maisha yako.Gharama kwenye maisha yetu ya kila siku inatofautisha umuhimu wa vitu.Gharama inaweza tofautisha vipaumbele,gharama inaweza tofautisha watu,gharama inaweza tofautisha aina ya makazi tunayoishi. Kila kitu kinatofautishwa na gharama,gharama inaamua yupi umuheshimu yupi umwashae.

Muda mwingi tumejikuta tunaingia kwenye gharama bila sisi wenyewe kutambua kwa sababu hatukuweka darubini zetu kuona mbali,Kuna mambo yanawezeka kuonekana ni rahisi kumbe yana gharama kubwa na kuna mambo yanawezekana yanaonekana ni gharama kumbe ni rahisi inategemea ni kipi umechagua kwenye maisha yako ya kila siku.

Watanzania wengi tupo tayari tununue viatu vya 2000 kila baada ya mwezi lakini hatupo tayari tununue kiatu cha 10000 kwa kila baada ya mwaka mmoja.Kuna mambo ukiyaangalia ni rahisi lakini gharama yake kubwa lakini kuna mambo ukiyaangalia kwa jicho la tofauti unakuta gharama yake ni kubwa lakini kumbe kwa muda mrefu ujao ni rahisi zaidi.

Mtanzania Yupo tayari ananunue vocha ya simu ya 500 kila siku kuliko anunue kifurushi cha 2000 cha wiki nzima.Sasa kwa muda mrefu nani mwenye faida nani mwenye hasara ndipo unapogundua Gharama ni Raisi kuliko Raisi kuwa Gharama kwenye maisha yako ya kila siku.

Mambo Machache yanayoweza kukusaidia kutambua kwamba "Raisi ni Gharama ,Gharama ni Raisi"

MUDA :
Ukitaka kujua jambo lolote ni Raisi au bi Gharama angalia kwa muda mrefu ujao linakuwaje.Mfano Unaponuanua Vocha ya 500 kila siku kwa wiki umetumia 3500 lakini unaponunua kifurushi cha Wiki ni 2000 unajikuta umeokoa 1500 ambayo unaweza kuipeleka kwenye mambo mengine.Piga mahesabu kwa muda ujao kwamba utakuwa umepata faida au hasara.

VIPAUMBELE  :  Mara nyingi watu wengi tuna vipaumbele vingi ambavyo muda mwingine havina ulazima kuwepo.Kuna jambo unaweza ukalifanya mara moja likakupa faida endelevu na kuna jambo unaweza ukalifanya mara moja likakupa hasara endelevu. Mfano Unapokunywa pombe kidogokidogo inaonekana ni kiburudisho na kichangamsho lakini kwenye maisha yako yajao tarajia kuuguza mifupa yako. Badala ya Kunywa Pombe leo ukaamua kuwekeza kwenye Mlo  Kamili kila Siku unajitengenezea mwili wenye afya na unaoweza kudumu kwa muda mrefu zaidi.

UWEKEZAJI
Kila siku,kila mara kuna mtu anafanya  uwekezaji kwenye jambo fulani  linaweza kuwa lina nguvu kwa sasa lakini linaweza likawa hasara kwa kesho yako.Linaweza kuonekana ni dhaifu kwa sasa lakini lina nguvu kwenye kesho yako.Ni Rahisi mtu ukimueleza leo nikupe nafasi ya kufanya kazi au nikupatie hela atakachokwambia cha haraka nipate hela nishike kwanza wakati natafuta kazi.Mtu kama huyu kwa muda huo anaonekana amepata faida lakini kwa muda mrefu ujao raisi yake inageuka kuwa gharama.Ni vyema kuchunguza na kutambua wapi unawekeza leo, Namna unavyowekeza kwenye muda wako,namna unavyowekeza kwenye akili yako,namna unavyowekeza kwenye uchumi wako itakusaidia kugundua kwamba Raisi ni Gharama ,Gharama ni Raisi ?

“  RAHISI NI GHARAMA,GHARAMA NI RAHISI ? “
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.