SOMO: FAIDA ZA KUOKOKA NA KUAMUA KUISHI MAISHA MATAKATIFU (BILA MICHANGANYO) BAADA YA KUOKOKA

Mwalimu Dickson Kabigumila.

FAIDA ZA KUOKOKA NA KUAMUA KUISHI MAISHA MATAKATIFU (BILA MICHANGANYO) BAADA YA KUOKOKA.

Na Mwl Dickson Cornel Kabigumila.

1. Unakuwa na uhakika wa kusamehewa dhambi zako zote; 1Yohana 2:1-2, 1Yohana 1:8-10, Ufunuo 1:4-5.


2. Unakuwa na uhakika kuwa dhambi zote ulizotubu kwa kumaanisha kuziacha zimesamehewa na kusahauliwa kabisa na Mungu; Isaya 1:18, Isaya 43:25, Zaburi 103:20.

3. Una uhakika wa kupata nguvu ya kuacha jumla kila dhambi iliyokuwa ikikutesa kabla; Warumi 6:6-11, Warumi 6:12-14, 1Petro 2:24.

4. Unapewa uwezo wa kufanyika kuwa mtoto wa Mungu kisheria; Yohana 1:12, 1Petro 2:9, 1Yohana 3:1-2.

5. Ukiwa na Yesu "tayari" wewe ni mwenyeji wa mbinguni;
Waefeso 2:19, 1Petro 2:9, Ufunuo 5:9.

6. Tayari UNA UZIMA WA MILELE ndani yako;
Yohana 3:16-18, Yohana 17:3, Yohana 5:24, 1Yohana 5:13.

7. Umebarikiwa tayari kwa baraka zote za rohoni (anazomilki Mungu), na ni zako wewe na Bwana Yesu mnazirithi pamoja.
Kila alichonacho Mungu ni chako wewe na Bwana Yesu.
Na wewe na Bwana Yesu mna haki sawa mbele za Mungu baba katika kurithi alivyonavyo;
Waefeso 1:3, Warumi 8:16-17, Wagalatia 4:6-7.

8. Yesu amekukatia "BIMA YA AFYA" msalabani. Ukiamini ni haki yako KUTOKUWA MGONJWA kabisa;
Isaya 53:4-5, 1Petro 2:24, Mathayo 8:16-17, Zaburi 103:3, Isaya 33:20-24, Isaya 35:8-10.

9. Uhakika wa ushindi, uhakika wa nguvu, na uhakika wa mamlaka dhidi ya NGUVU ZOTE ZA GIZA; Wakolosai 1:13, 1Petro 2:9, Yohana 8:12, Isaya 60:1-3, Zaburi 91:2-13, Luka 10:19, Luka 9:1-2, Hesabu 23:23.

10. Uhakika wa ulinzi wa Ufalme wa Mungu kwako;
Zaburi 34:7, Zaburi 91:2-13, 1Petro 1:5, Kutoka 23:20.

11. Uhakika wa hatma/ mwisho mwema;
Wafilipi 1:6, Wafilipi 2:13, Yeremia 29:11, Mithali 4:18, Ayubu 8:7, Ayubu 42:12-17.

12. Uhakika wa maisha marefu;
Yohana 11:25-26, Zaburi 91:14-16, Ayubu 42:16-17, Isaya 65:19-20.

13. Uhakika wa kuweza "kutembea na Mungu" kama best friend wako kila mahali na kila siku, Huku akifanya mambo ya kushangaza kupitia wewe na pamoja na wewe;
1Samweli 3:19, Matendo 10:38, Yohana 3:2, Marko 16:20, Kutoka 33:12-17.

14. Uhakika wa wewe mwenyewe kuwa "ishara na ajabu" kwa kizazi chako na kufanya dunia ijue kwamba ulikuwepo (LEGACY);
Isaya 8:18, Marko 16:17-18, 20, Matendo 1:8, Matendo 5:12-16, Matendo 6:8, Matendo 8:5-13, Matendo 19:11-12.

Wokovu ni mtamu sana.
Ukiokoka, huwezi kuyapata haya katika uhalisia wake mpaka utakapoamua kuwa mtakatifu.
Kiwango cha ubora wako kinategemea uamuzi wako wa kuwa MTAKATIFU na kujitenga na dhambi (2Timotheo 2:20-26).

Zingatia hili; Usikubali Shetani akudanganye kusoma ujumbe huu bila kusoma na maandiko yaliyomo. Siri kubwa ya kuwa mtu wa imani ni kufuatilia na kusoma maandiko. Hakikisha umeyasoma vizuri na kwa utulivu.

KWA WAKAZI WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO MWALIMU KABIGUMILA ATAKUWA HUKO soma tangazo hili chini


Mwl Dickson Cornel Kabigumila
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.