SOMO: FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA BARAKA ZA AGANO NA MUNGU (Sehemu ya mwisho) - MWALIMU MWAKASEGE

Leo tunamalizia sehemu ya mwisho ya neno hili kama lilivyofundishwa na mwalimu Christopher Mwakasege katika semina ya neno la Mungu iliyofanyika mkoani Dodoma. Kama hukusoma sehemu zilizopita za neno hili basi BONYEZA HAPA vinginevyo endelea na sehemu ya mwisho chini.DAY 7&8
HATUA ZA KUKUSAIDIA KUONA BARAKA ZINATOKEA KATIKA MAISHA YAKO NA UNATEMBEA NAZO.
5. Omba Mungu asimamie mazingira yanayotokea wakati mtu anayehusika na agano la urithi anapokufa. Ebr 9:16-17.
•Agano la urithi limebeba vitu ambavyo warithi wanatakiwa kupata.
•Kifo cha mtu aliyekuwa kwenye agano kina nguvu. Mwa 25:11, 27:41, 50:14-20.
•Kifo cha Yakobo kiliachilia matengenezo katika nyumba yake.
•Agano la urithi lilipo lazima mauti iwepo kuhamisha urithi. Kut 1:6-8, Josh 1:2-3
•Sadaka ya shukrani baada ya mtu kufa inamfanya Mungu kutoa hekima ya kuishi bila ya mtu yule aliyefariki.
6. Fuatilia urithi waliopangiwa watumishi wa Mungu. Hes 18:19-31, Kumb 12:18-19.
• Mungu anawatunza tofauti na watu wengine.
Hakutaka watu hawa wategemee urithi/ sadaka au watoa sadaka.
Mambo muhimu ya kuzingatia:
•Nafasi
Nafasi ya nabii ina baraka zake. Atakupa maelekezo ya kufanya katika nafasi hiyo.
•Utii
Baraka zako zipo katika mwisho wa kutii kwako
•Kusudi la kutumika( motive). Math 6:33
Ufanyapo hayo:
•Upako utakuwa juu yako
•Atahakikisha sadaka zinakuja( Mungu anakuinulia watu)
•Mungu ayakunyanyulia malaika.
•Lazima uone faida katika kumtumikia Mungu. Mal 3:13-15, 2:1-9.
7. Muombe Mungu akukutanishe na Joshua wako. Josh 1:6
Maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa urithi wao.
•Kurithisha: kukuwezesha kurithi/ kukaa ndani ya urithi kiasi kwamba hata Joshua akiondoka utatembea na huo urithi.
•Muombe Mungu amtunze Joshua wako ili akufikishe kaanani yako.
8. Shindana hadi ushinde kinachotafuta kukuzuia kurithi baraka zako. Ufu 21:5-7
•Yeye ashindaye atayarithi haya... Usipo shinda huwezi kurithi. Ebr 3:16-19, Gal 3:9.
•Baraka ya mtumishi ipo pale amalizapo kazi. 2Sam 17:1-2
•Ni hatari kuchoka kabla ya kumaliza kazi. Adui husubiri pale tunapochoka.
Ufu 21:7, Yoh 7:37 ukipata kiu nenda kwa Yesu. Ukijenga uhusiano wako na Mungu atakata kiu yako.
•Kama kisima chako kimefukiwa fukua. Mwa 26: 12-33.
Mwisho.. Barikiwa.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.