SOMO: KIBALI - MCHUNGAJI JOHN KILIMA


SOMO: KIBALI
Na: MCH. JOHN KILIMA

Kibali ni mvuto au upendeleo alionao mtu ili unapofika wakati wa Mungu unapofika wa kuinuliwa kwake watu waliowekwa na Mungu kwa ajili ya kumuinua waonekane. Kibali kinaweza kuibwa au kufunikwa ili mtu asionekane.
Mhubiri3:1-8
Kila jambo na wakati wake, hivyo unapofika wakati wa kuinuliwa kwake kibali chake huonekana.
Wanaoweza kuiba au kufunika kibali ni mashetani lakini leo tutawashughulia kwa Jina la Yesu.
Ufunuo12:7

Baada ya vita mbinguni shetani/ibilisi akatupwa hata nchi na biblia inasema muda wake ni mchache hivyo anafanya kazi yake kwa bidii sana.
Shetani au pia joka kuu la zamani, Yesu pia ana majina mengi mkate, wa uzima, mwana wa Mungu, ufufuo na uzima, Mfalme wa wayahudi niko ambaye niko, Jehovah n.k kitu kilichowachanganya waliokuwa wakimshitaki.
Yupo Mungu wa Waislamu alifahamika kwa jina la al-mukadir yaani wa zamani
Kutoka3:3
Hapo Mungu alijitambulisha kama niko ambaye niko yaani ukimuita kulingana na hali uliyonayo ndivyo atakavyotokea.

Mfano: Jehovah rafa-mponyaji
Jehova elgibo-mwenye nguvu
Jehovah shamah- Mungu yuko hapa
Shetani naye kwakuwa ni mungu wa dunia hii, hufanya mambo ambayo watu watamuabudu.
Shetani baada ya kutupwa akatupwa akatafuta namna ya kuleta ufalme wake kwa kujiungamanisha na wanadamu. Aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye na aliyeungwa na Kristo ni roho moja naye.
1Wakorintho6:16-17
Shetani ameijua njia pekee ya kujiungamanisha na wanadamu ni kupitia ndoa. Wawili wanaweza kuwa mwili mmoja.

Hati ya ndoa ya kishetani huwepo ili kumpa shetani uhalali wa kujiungamanisha kwake na mwanadamu. Lakini Yesu ameishaifuta hati hiyo msalabani.
Kolosai3:13
Kingine ni pete, nayo humpa shetani uhalali wa kujiunga na wanadamu. Wengine huokota pete na kuzivaa au hupelekwa kwa sonara na watu wengine hununua pete hizo bila kujua zilitoka wapi na kuleta matatizo maishani mwako, wakati wa Mungu unapofika ili uinuliwe unakuwa huonekani.
Vyanzo vya matatizo ni katika ulimwengu wa roho wa giza, hivyo ili kuondoa tatizo ni kwenda kwenye ulimwengu wa roho na kukatilia mashetani ambayo ndio vyanzo vya matatizo.
Unaweza ukaishi na watu ukajua ni wakawaida sana lakini ndani yake ni shetani kamili.
Kuna wakati shetani ametuwekea chapa zake ili tusivuke kuelekea tunakotakiwa ndio maana Paulo akasema amebeba chapa za kristo mwilini mwake.

Galatia6:17
Ufunuo17:1-6
Shetani anayevuvia uovu, uzinzi, na matukio mabaya ni malkia wa mbingu ambaye wengi wwamemuabudu wakidhani ni bikira maria. shetani kwa kujua watu wana kibali toka kwa Mungu amewawekea chapa zake ili wasije wakapata kuinuliwa wakati ukifika.
Kwa damu ya Yesu nafuta chap azote ambazo shetani ameniwekea mahali popote kwenye mwili wangu chapa za magonjwa,chapa ya uharibifu, chapa za kuachwa au kukataliwa nazifuta zote kwa Damu ya Yesu imeandikwa nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao nayafuta mashetani yote yaliyogeuka kuwa chapa za kishetani ili nikose kibali kwa Jina la Yesu.

AMEN
UFUFUO NA UZIMA -TANGA

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.