SOMO: MUNGU ANAJUA UNAYOPITIA - KING SAM

Mtumishi King Sam

SHALOM MWANA WA MUNGU ALIYE HAI;
MUNGU ANAJUA NJIA YA WEWE KUTOKA KATIKA MAHALI ULIPO ANAJUA NJIA YA WEWE KUFANIKIWA NAJUA MUDA WA WEWE KUPATA MTOTO,YOTE MUNGU ANAJUWA USILAUMU KATIKA HALI ULIYO NAYO MAANA ANAJUA UTATOKA TU KATIKA JINA LA YESU,

ANGALIA WANA WA ISRAEL WALIPOKUWA UTUMWANI WALILIA MUNGU AKASIKIA KWA SABABU YA MATESO WALIYOYAPATA MISRI LAKINI MUNGU ALIKUWA ANAJUA NA KUINGIA KWAO UTUMWANI biblia inasema hivi
Mwanzo 15:13
BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.
14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.
ANGALI WAKATI WA KUTOKA ILIKUWAJE
Kutoka 12:35
Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.
36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara.

INA MAANA ALIKUWA ANAJUWA NA MUDA WAO WA KUTOKA HUKO NA NI NANI ATAWAOTOA NDIYO MAANA BIBLIA INASEMA HIVI
Yeremia 1:5
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

HATA LEO MUNGU ANAJUWA WEWE YALIYOKUPATA NA NJIA YA KUTOKEA NA MUDA KAMA NI KUFANIKIWA AU KUOLEWA AU KUPATA MTOTO AU KUPOA HUO UGONJWA AU KUPATA KAZI NK MUNGU ANAJUWA NA ALIJUWA UTAPITIA UNAKO PITIA AU ULIKOPITA USIOGOPE KATIKA JINA LA YESU UTASHINDA AMEN
TUNAWEZA ONA HATA KWA AYUBU MUNGU ALIKUWA ANAJUWA SHETANI ATAMTESA AYUBU LAKINI KWA SABABU ALIMJUWA AYUBU ALIJUWA ATASHINDA TU PAMOJA NA MATESO KWA HIYO MUNGU ANAJUWA PAMOJA NA MATESO UNAYOPITIA UTATOKA TU HUKO UTASHINDA KATIKA JINA LA YESU,Yesu alisema ugonjwa Wa Lazaro si Wa mauti Bali ni kwa ajili ya utukufu Wa Mungu
Yohane 11:4
Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.
AYUBU YEYE ALICHOFANYA HAKUMKOSEA MUNGU KWA MAPITO YAKE MAANA ALIMJUWA MUNGU ATAMPONYA
Ayubu1:22
Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu
NDUGU YANGU KATIKA YESU KRISTO YESU ALIKUJA AKAFA MSALABA KWA AJILI YAKO ILI UPONE UWEKWE HURU UFANIKIWE KATIKA YESU MUNGU ALIJUWA KUPITIA MSALABA UTAKOMBOLEWA ANGALI MFANO WA YESU ULIVYO WAKOMBOA ISRAEL
Hesabu 21:8
Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.

NDUGU YANGU MWANALIYE YESU UTAPONA UTAFANIKIWA KATIKA JINA LA YESU MUNGU ANAJUWA NA ALIJUWA KATIKA MAPITO YAKO YOTE NA AMEWEKA NJIA YA WEWE KUTOKA NA KATIKA NJIA HIYO KUTAKUWA NA MAFANIKIO UPONYAJI USHINDI KATIKA JINA LA YESU AMENI
USILAUMU Bali MSHUKURU YESU MWAMBIE ASANTE YESU MAANA KATIKA MAPITO HAYA KUNA USHINDI KATIKA NJIA HII KUNA USHINDI USILAUMU KWA AJILI YA MME AU MKE AU RAFIKI AU WAZAZI AU KAZI NK BALI SHUKURU MUNGU KWA YOTE KATIKA JINA LA YESU MAANA MUNGU ANAJUWA UTAPITA NA KUNA USHINDI KUNA MAFANIKO
Ubarikiwe katika jina la Yesu amen

King Sam
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.