SOMO: NGUVU YA MANENO, FAIDA NA ATHARI ZAKE (2)

Askofu Sylvester Gamanywa
Jumatatu iliyopita (soma hapa) nilikudokeza mada inayohusu habari ya NGUVU YA MAWAZO. Humo tulichambua mambo kadhaa yakiwemo mawazo chanya na mawazo hasi. Na kisha tulichambua habari za “ngome za mawazo” ambazo huzalisha “falsafa za kibinadamu” na “Nadharia potofu za kidini.” Leo nimeona nikupatie muhtasari wa sehemu ya pili ya ujumbe  wenye kichwa kilichoko hapa juu kisemacho NGUVU YA MANENO, FAIDA NA ATHARI ZAKE: Hii haina maana kwamba tumekatisha ujumbe wa “nguvu za mawazo”; la hasha. Vitu hivi vinahusiana sana kiasi kwamba utangulizi wa leo utakuwezesha kuunganaisha mambo magumu yawe mepesi zaidi kwa kuujua mfumo wa utendaji kati ya mawazo na maneno.


Utangulizi kuhusu tafsiri ya Maneno

Msamiati wa “maneno” ni uko katika wingi. Umoja wake ni “Neno”. Kimsingi, Neno katika asili yake lina sura tatu zinazolitambulisha Neno na utendaji wake. Na kila sura ina majukumu yake maalum tofauti na nyingine ingawa kusudi lake ni moja, kulifanya neno liwe na nguvu za kiutendaji.

Hay tukirejea msamiati wa maneno, leo tutaanza kujifunza aina tatu za maneno. Kuna maneno na binadamu. Kuna maneno ya Mungu. na Kuna maneno ya shetani. Kwa sababu za kiutaalamu nitapenda tuelimishane kuhusu nguvu za maneno ya binadamu kwanza, na sehemu ya pili tutapitia nguvu za Maneno ya Mungu.
“Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” (MT.12:37)
“Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.” (Mith.18:21)
Mpendwa msomaji, hapa tunaona kwamba, maneno yako na yangu ya nguvu za kushangaza japokuwa sisi wenyewe hatuyapi uzito unaostahili. Na ndiyo maana tunaathiriwa na kuangamizwa na maneno yetu wenyewe, pasipo hata kujua ni kwa jinsi gani tunaathirika kwa maneno yetu wenyewe.
Kimsingi, kazi kubwa ya maneno ni kwa ajili ya “mawasiliano” katika ya binadamu wenyewe, au binadamu na Mungu au binadamu na viumbe wengineo. Likini tukitaka kufahamu siri ya nguvu za maneno ya binadamu hatuna budi kujua kiuambile maneno yameumbwa kwa jinsi gani na utendaji wake ni wa namna gani.
Mahali pa kuanzia ni kutambua kwamba “Neno la binadamu lina sura 3 za kiutendaji. I) Wazo II) Andiko III) Sauti/tamko Mambo haya 3 yanawakilisha sura za Neno. Haya basi, unaona katika ujumbe huu tunakutana na msamiati wa neno “wazo”? Ndiyo maana nikaona nikuletee ujumbe kamili utakaokusaidia kuyatofautisha mamabo yanayoingiliana sana kama “Maneno” na “Mawazo” Haya hebu tuendelee na uchambuzi wa “Maneno”
Pengine ni muhimu pia kujikumbusha kwamba, binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu na sura ya Mungu. Katika kuumbwa kwa mfano wa Mungu binadamu ameumbiwa sehemu maalum tatu ambazo ni i) mwili ii) Nafsi, na iii) roho.
Katika sehemu hizi tatu za binadamu sehemu ya Nfasi ndiyo kiungo kikuu cha mawasiliano kati ya binadamu na ulimwengu wa asili. `Na ndiyo maana nafsi nayo  imegawanyika katika sehemu 3 ambazo ni i) akili ii) hisia iii) utashi. Sehemu hizi tatu ndizo zinaifanya Nafsi ya binadamu ihusike katika matumizi ya maneno. 
Mathalan, katika akili za nafsi ya binadamu ndipo “Neno” la bnadamu linaishi katika mfumo wa “wazo”. Lakini binadamu akitaka kuwasiliana na ulimwengu wa asili inambidi atumie sehemu yake ya kimaumbile ambayo ni “sauti” ili kulitoa “Neno” kutoka kwenye mfumo wa “wazo” lisikike katika “mfumo wa sauti” na ndipo mawasiliano katika ulimwengu wa asili yanakamilika.
Lakini kwa sababu bidanamu ambaye anaishi katika ulimwengu wa asili anaisha katika mazingira yenye kumfanya asahau upesi, ili kuweka kumbukumbu za mambo yake katika ulimwengu wa asili anatumia sura ya Neno ambayo ni “andiko”

Kila Neno aliwazo binadamu au kulisema akitaka kulikumbuka katika uliwengu wa asili lazima alitunze katika kumbukumbu ya maandishi. Hapa tunamwona binadamu katika nafsi, anafanya mawasiliano kwa sura 3 za maneno ambayo kila sura ina utendaji wake ili kukamilisha mchakato wa mawasiliano.
Sura 3 za maneno ya Mungu na kazi zake

Baada ya kupitia uchambuzi wa maneno ya binandamu, sasa tunaingia katika kuchambua sura 3 za mameno ya Mungu na kazi zake.

Utakumbuka kwamba, binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu na sura ya Mungu. Mojawapo ya sehemu ambazo binadamu anafanana sana na Mungu, ni katika suala la nguvu na matumizi ya maneno. Hebu tujifunze kwa Muumbaji wetu na kujua nguvu zilizomo katika maneno yake.

Tuanze kujifunza kwamba, Maneno ya Mungu yako katika mfumo wa “Mawazo”, na “Maandiko” na pia katika “sauti”! Ushahidi wa “Mawazo ya Mungu” tunasoma katika maandiko yafuatayo” “Mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.” (ISA.55:8)

Kisha sura ya pili na Maneno ya Mungu katika mfumo wa “Andiko” tunasoma maandiko yafuatayo:“Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho…..” (2 Tim.3:16 Na sehemu ya 3 ya maneno ya Mungu katika “mfumo wa sauti” tunapata ushahidi wa maandiko yafuatayo: “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”(Rum.10:17)
 Sasa napenda tuanze kuchambua vipengele hivi 3 kimoja baada ya kingine kama ifuatavyo:
1.         Mawazo ya Mungu
Mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.” (ISA.55:8)

Mungu wetu ana mawazo. Kwanini, kwa sababu Mungu ana Nafsi na mawazo hukaa katika Nafsi, katika kitengo cha akili. 
Mawazo ya Mungu, yako juu saa kuliko mawazo yetu. Mawazo ya Mungu ni makamilifu sana kuliko mawazoo yetu. Mawazo ya Mungu ni roho yenye uzima tofauti na mawazo yetu.
Mawazo ya Mungu yamebeba nia ya Mungu, na tabia yake, na ndio chimbuko la nguvu ya ubunifu wa kiungu. Kila jambo jipya huzaliwa na wazo jipya, na kila wazo jipya la Mungu limebeba uhai na uzima wa jambo hilo. 
Mungu anataka sisi  tuyajue mawazo yake, ili kujua nia yake na tabia, Lakini zaidi sana Mungu anataka tukiyajua mawazo yake, tuyaruhusu yaingie katika akili zetu ili yaangushe ngome za mawazo potofu, dhaifu na ya uharibifu yaliyomo katika akili zetu
Itaendelea toleo lijalo

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.