SOMO: UBATIZO NI HAKI YAKO (Sehemu ya mwisho) - MCHUNGAJI MADUMLA                              Mchungaji Gasper Madumla katika moja ya mahubiri yake.

Kusoma sehemu ya kwanza ya somo hili BONYEZA HAPA

Bwana Yesu asifiwe,

Ubatizo ni silaha ya kuvunja kila aina ya vifungo vya giza. Haijarishi ni vifungo vya namna gani,lakini nakuambia ikiwa utabatizwa katika Roho na kweli,ni lazima vifungo vikuachie. Sikia; Wapo watu waliokuwa wakiteswa na nguvu za giza sana,lakini walipoakata shauri,wakabatizwa katika ubatizo wa Yesu,walipokea uponyaji saa ile ile.

Hivyo,usidharau ubatizo ulio sahihi,ni dawa kwako na pia ni haki yako.

Shetani ujaribu sana kuwafunga watu wa Mungu wasibatizwe katika ubatizo aliobatizwa Yesu,yaani ubatizo wa maji mengi na wenye kusimamiwa na nguvu za Roho mtakatifu.Ngojanikupe mfano kidogo kabla sijaendelea;Mtu mmoja aliokoka,kisha akaadhimia abatizwe,alipotaka kubatizwa gafla ndugu zake pamoja na mama yake mzazi akamzuia na kumuambia kwamba ” …vyoote ufanye katika imani yako ya kikristo,lakini sio kubatizwa…” Hivyo mtu huyu alikuwa na ukinzani mkubwa sana kutoka kwa ndugu zake,ilikuwa ni kama vita kwake. Na walichokuwa wakikizuia si kingine bali ni ubatizo maana walijua akibatizwa tu basi wamemkosa katika mabaya yao waliyoyapanga.Lakini mtu huyu akafanikiwa kubatizwa,na tagu siku hiyo hakutembea tena katika vifungo vya magonjwa.Umeonaa? Ndio maana ninakuambia ubatizo ni silaha!

Shetani uelekeza mashambulizi yake katika ubatizo tena hujaribu kuwavuruga hata baadhi ya wachungaji kwa habari ya ubatizo,kiasi kwamba wachungaji wasione umuhimu sana ya kubatiza waamini wao katika Roho na kweli,na hatimae hujikuta wakiwabatiza kwa kuwanyunyuzia maji,au wakiwabatiza katika maji mengi pasipo kuwepo kwa mafundisho ya kina kuhusu ubatizo.Hii ni hatari katika kanisa la leo!

Ubatizo huja baada ya kuamini neno la Mungu,tazama Simoni yule aliyekuwa mchawi. Biblia inasema;

” Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.‘‘ Matendo 8:13Mch. Gasper akikabidhi vyeti kwa wabatizwa,akiwa ameambatana na wachungaji Mch.Juliana kushoto kwake,pamoja na wachungaji viongozi kanisa la Beroya bible fellowship church.

Oooh kumbe!

Maana yake;Ili mtu aamini kweli (Neno) ni lazima neno la Mungu lihubiriwe na kufundishwa kiundani.Kwa lugha nyingine ni kwamba ikiwa patakuwa hakuna neno kamilifu la Mungu basi mtu hawezi kuamini impasavyo,na mtu huyo anakuwa hana vigezo vya kubatizwa ingawa ni haki yake. Simoni alipobatizwa,alipokea nguvu ya muambatano ndiposa akashikamana na Filipo ingawa yeye mwenyewe Simoni alikuwa mpenda pesa aliyepitiliza sababu alitaka auziwe karama ya Mungu kwa pesa. Macho ya Simoni yalifumbuka mara baada ya ubatizo maana alianza kuona ishara na miujiza mikubwa ikitendeka yamkini hakuwai kuona kama ailivyoona baada ya ubatizo,kwa sababu ubatizo ulimfumbua macho yake apate kuona uweza wa BWANA jinsi ulivyo mkuu.

Na ndivyo jinsi ilivyo hata sasa,kama ukiipokea haki yako ya ubatizo basi ujue BWANA atakufungua macho yako na kuanza kuona nguvu ya Mungu kwa namna yake tofauti kabisa na vile ulivyokuwa ukioona hapo awali kabla ya ubatizo.Zipo aina mbili za ubatizo kwa mujibu wa biblia;

* Ubatizo wa toba,(Ubatizo wa Yohana),Ubatizo wa maji mengi.

*Ubatizo katika Roho mtakatifu ( Ubatizo huu huja mara baada ya ubatizo wa toba)

Imeandikwa;

” Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.
Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu. ” Matendo 19:3-8

Kaitika andiko hilo,biblia imeweka wazi juu ya aina mbili za ubatizo yaani ubatizo wa toba,na ubatizo katika Roho mtakatifu. Biblia inasema;Watu wale baada ya kubatizwa katika ubatizo wa Yohana,Paulo akawaambia watu wale wamuamini Yesu Kristo kiboko ya wote kisha ” waliposikia haya ”wakabatizwa katika Roho yaani katika jina la Bwana. Neno ” waliposikia haya”maanake walihubiriwa ndio maana waliweza kusikia,maanake walifundishwa neno ili waamini kisha wabatizwe katika Roho. Paulo akawabatiza katika Roho kwa kuwawekea mikono kisha Roho mwenyewe akawa kazini kumuhudumia kila mmoja wao,wakanena kwa lugha na kutabiri. Kipawa cha ujazo wa Roho mtakatifu ni ahadi yako,lakini kwanza pokea haki yako ya ubatizo!

Sikia;

Hata mitume,hawakuruhusiwa watoke kufanya kazi ya BWANA pasipo kupokea haki yao ya kubatizwa katika Roho. Biblia inasema;

” Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. ” Matendo 1:4-5

Mitume walipobatizwa tu katika Roho,ndipo tunaona wakiwa tayari kwa kazi ya Bwana kwamba watoke Yerusaremu.

Hili ni fundisho kwako wewe mtumishi wa Mungu,kwamba hutakiwi kuanza huduma kabla ya kupata haki yako ya ubatizo wa toba,na ubatizo katika Roho sawa sawa na mitume wa kwanza jinsi walivyopokea ubatizo huu. Tazama nguvu ya Mungu iliyopo katika kanisa la kwanza,ilikuwa si ya kawaida sababu mitume walitembea katika mpangilio sahihi wa kihuduma sawa sawa na wito wao.

Ni furaha yangu siku ya leo,kwako wewe mpendwa usomaye fundisho hili; kwamba upokee haki yako hii ya ubatizo wa maji mengi ule wa toba wenye kuzika magonjwa yako yote na kufufuka na Yesu,pia ubatizwe katika Roho ili karama yako ichochewe tarayi kwa kutumika katika Roho na kweli.Basi waweza nipigia sasa kwa namba yangu hii; 0655-11 11 49.

UBARIKIWE

MWISHO.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.