TUNACHAGUA KUFUTWA MACHOZI PAMOJA NA EDNA KUJA


Tunatumai kwamba u buheri wa afya mdau wa GK. Kwa Jumapili ya wiki hii tunachagua kufutwa machozi pamoja na Edna Kuja, ambaye anazindua DVD yake kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl (Ubungo Plaza).

Inawezekana umetulia tu na ukadhani kwamba mambo yanajipeleka yenyewe, lah! BWANA Yesu ndiye mpelekaji wa mambo yote, anatuondolea aibu, amechukua mizigo ya dhambi zetu, na kutuhuisha kwa upya.

Tuungane na Edna Kuja kwenye chaguo la leo, na pia kwa mkazi wa Dar es Salaam tukutane ukumbini kuanzia saa saba na nusu mchana ambapo waimbaji zaidi ya 25 watakuwepo kuimba, baadhi yao ni kama vile Jessica BM, Lilian Kimola, Angel Benard, Lilian Mariki, David Banali, ALFA Melody SDA, Gazuko Jr, Ukombozi Msasani Choir, Ambwene Mwasongwe, Miriam Mauki, Furaha Isaya, Michael Komba (Arusha), Joshua Silomba, MC Mkolosai, Ester Shedafa, Betty Lucas (Mwanza), Loveness Mwaikaja (Singida), na wengineo wengi, ili mradi sifa na utukufu ni kwa BWANA Yesu.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.