USIREJEE KWA MUNGU NA GB ALIZOKUPA, TUKUTANE VICTORIA SERVICE STATION


Ni kwa wale tu waliofika ndani ya ukumbi wa Victoria Service Station ndio wanaopata vitu adimu kila iitwayo Jumapili kupitia Sunday Celebration, tukio ambalo huandaliwa na Glorious Worship Team.

Kwa Jumapili iliyopita, somo mahsusi kutoka kwa Eric Shigongo liliwagusa vilivyo washiriki, kwani walikumbushwa kutorudi kwa Mungu na GB alizowapa. Kipawa ulichonacho shurti ukitumie kwa manufaa ya ufalme wa Mungu, usikubali kufa na maarifa na jambo ambalo Mungu ameweka ndani yako. Pale unapokizungumza hufanyika uponyaji tosha kwa watakaosikia.

Basi hiyo ni kwa kifupi tu kati ya mambo uliyokosa Jumapili iliyopitta. Tukutane Jumapili hii tarehe 17 kwenye ukumbi wa Victoria Service Station, ambapo pamoja na waimbaji mbalimbali kuhudumu kama vile Christina Shusho na Vocapela, atakuwepo pia Eric Shigongo kuzungumza nawe.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.