CHAGUO LA GK: TUABUDU KWA SONG OF THE LAMB KUTOKA WORSHIP MOB

©Worship Mob/fb.
Tunatumai umekuwa na Jumapili yenye baraka mdau wa GK. Leo ikiwa ni Jumapili ya mwisho wa mwzi wa sita, tayari kabisa kuanza nusu ya miezi iliyosalia kumaliza mwaka, chaguo la GK linatoka kwa kundi la kuabudu kutoka Colorado Springs, Colorado nchini Marekani, Worship Mob.

©Worship Mob/fb
Kundi hili ambalo ni maarufu sana katika kuabudu live (live worship), lina vipaji wahudumu mbalimbali, ambapo leo tunakupa wimbo mmoja unaoongozwa na Harvest Bashta, Song of the Lamb.

Licha ya kwamba wanamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji, kundi hili lenye waimbaji zaidi ya 100 kutoka zaidi ya makanisa 25, linaamimi kwamba kama ambavyo Yesu alijitoa msalabani kwa ajili yetu, ndivyo ambavyo tunapaswa kujitoa kwake kwa njia ya kumuabudu.

Nyimbo zao hutolewa bure kwa watu wote, bila mauzo. Na kama wewe ni muabudu, basi u sehemu ya familia ya Worship Mob. Barikiwa na BWANA Yesu.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.