CHAGUO LA GK TUPO NA WAIMBAJI WA VIWANGO NCHININi jumapili ya kwanza mwezi June mwaka 2015, katika chaguo la GK tumekuchagulia nyimbo kutoka moja ya makundi yaliyovuma mara baada ya kutoa toleo lao la kwanza. Tumekuchagulia waimbaji TM Music la jijini Dar es salaam, kundi hili ni mkusanyiko wa waimbaji kutoka kwaya na madhehebu mbalimbali jijini humo ingawa asilimia kubwa ni kutoka kanisa Sabato. Kwaya hii mpaka sasa ina album tatu, Tutamwona Mwokozi, Sioshwi Dhambi pamoja na Nyota njema ya Bethlehem. Tumekuchagulia  uburudike na album yao ya kwanza 'Tutamwona Mwokozi'. Tunatumaini utabarikiwa utazamapo na usikilizapo. Tunakutakia jumapili njema

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.