CHAGUO LA GK UJUMBE ADIMU KUUPATA KWA WAIMBAJI WA SASAChaguo la GK siku ya leo tumerejea tena jijini Arusha tunakokutana na kwaya kongwe ya Tumaini Shangilieni ambao licha ya kupiga muziki mzuri pia jumbe zinazopatikana katika nyimbo zao ni adimu kuzipata kwa waimbaji binafsi ama kwaya za nyakati hizi ambazo zimeegmea kuimba nyimbo ambazo zimelenga upepo unavyokwenda kwa kufuata maneno yaliyopo mitaani.

Wimbo tuliokuchagulia unaitwa 'Machozi' ni hakika utabarikiwa na wimbo huu ambao unapatikana kwenye toleo lao la video walilotoa mapema mwaka jana iitwayo 'Nisamehe'. Wimbo huu wa kutafakari matendo makuu ya Mungu na jinsi tunavyomtegemea katika yote, utakubariki na kukuhuisha kwa mara nyingine tena. Tukutakie baraka za Mungu na jumapili njema.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.