HOUSE OF TALENT NDANI YA SUNDAY CELEBRATION LEO


Kwa wakazi wa Dar es Salaam waliopata neema ya kufika ndani ya ukumbi wa Victoria Service Station, hakika wanaweza kukuelezea ni kwa namna gani wanabarikiwa na huduma ya Glorius Worship Team inayofungua vijana kwa namna mbalimbali.

Na kwa Jumapili ye leo kama ilivyo ada, GWT wako tena mahala pale wakisubiri muda utimu ili waanze kuhudumu. Cha kufanya ni kuamka pale ulipo na uweze kuzifikia baraka zako. The Joshua Generation wapo, Sam Batenzi yupo, na mzungumzaji mkuu, Eric Shigongo naye yupo.

Mafundisho, kusaka vipaji, kusifu na kumuabudu Mungu na mijadala ni sehemu tu ya yatakayojiri. tukutane Victoria Service Station kuanzia saa tisa mchana.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.