JIONEE PICHA ZA KWAYA YA EFATHA UHURU MORAVIAN AMBAO WAPO NCHINI UJERUMANI KIHUDUMAKama ulivyojionea video fupi ya Efatha Uhuru Moravian kwaya katika ukurasa wetu wa Facebook, wakiimba kwenye tamasha nchini Ujerumani wiki iliyopita. Zifuatazo ni baadhi tu kati ya picha nyingi tutakazokuwekea kwenye GK ili ujionee huduma ya kwaya hiyo ambayo ipo nchini Ujerumani kwa mwaliko wa makanisa ya Kiprotestant ikitarajiwa kurejea nyumbani mwishoni mwa wiki ijayo.

Efatha ambao wamefikia katika mji wa Stuttgart wiki iliyopita, hii leo wapo Hapenham nchini humo ambako wanatarajia kuendesha semina ama darasa kuhusiana na muziki wao na wakiafrika kiujumla. Kwaya ya Efatha imetamba na wimbo wa 'Twaomba Amani' ama kwa jina lingine 'Mafarakano' ni moja kati ya kwaya bora kabisa ya kanisa la Moravian Tanzania. Ambapo kwaya hiyo yenye waimbaji zaidi ya 40 imewakilishwa na waimbaji 25 tu nchini Ujerumani wakiongozwa na mwenyekiti wao bwana Nsajigwa Tufingene.

Baadhi ya waimbaji wa Efatha mara baada ya kuwasili Ujerumani
Simon Abel mmoja wa viongozi wa kwaya akiwa amepozi 
Dennis Chando akiwa na Fred Mwamakula mbele ya jukwaa wakijiweka sawa kumtukuza Mungu
Mwenyekiti wa kwaya Nsajigwa mkono wa kushoto akiwa na mpiga ngoma Johnson 


Efatha mitaani
Simon na Fred wakikatiza mitaa
Wana Efatha wakisubiria Mwakyembe (usafiri wa treni mwe)
Efatha katika matembezi kujionea mazingira

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.