JPILI HII NI ZAMU YA FLORA MBASHA NDANI YA UBUNGO PLAZA


Huenda akilini una kumbukumbu ya Flora Mbasha mnamo Disemba 2014, ambapo ndio mara ya mwisho kufanya tamasha, kumsifu na kumuabudu Mungu. Awamu hii mambo yako tofauti. Kama kwa kipindi chote hicho hujawahi kumuona Flora, basi kwa hivi sasa tambua kwamba anapopanda jukwaani, kuna timu kubwa nyuma yake - timu ambayo kazi yake ni moja tu. Kuhakikisha uwepo wa Mungu unashushwa kupitia muzii live.


Nipe nguvu ya kushinda ndio album ambayo itakuwa ikitambishwa katika mfumo wa sauti na picha za sauti pia (video).

Akizungumza na GK, Flora ambaye anaisubiri tarehe 14 kwa shauku kubwa kwenye hoteli ya Ubungo Plaza kuanzia saa nane mchana, anaeleza kwamba ataimba nyimbo zote live siku hiyo, na kwamba yeye huwa hafanyi matamasha kwa mazoea, na kwamba mgeni rasmi siku hiyo ni BWANA Yesu.

tayari hadi hivi sasa waimbaji kadhaa wameshaelezwa kumsindikiza Flora siku hiyo, wakiwemo Furaha Isaya, Mwanamapinduzi, Elizabeth Ngaiza, Madam Ruti Benson, Tumaini Njole, Edson Mwasabwite, na wengine wengi lakini kubwa zaidi ni Mahanaim Band.

TIKETI SASA ELFU KUMI TU
Tiketi (ambazo zinapungua kwa kasi tayari), zimefikia hatua ya kupunguzwa bei hadi kufikia shilingi elfu kumi ili basi wale wapenzi wa Flora Mbasha wapate kufika kwa wingi zaidi katika kulisifu Jina la Mungu.


Tazama video ifuatayo kuona namna Flora alivyochangamka pamoja na timu yake.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.