PICHA 364 KILICHOJIRI SACRIFICE OF PRAISE CONCERT MSIMU WA PILI TANGA

 
Sacrifice Of Praise Africa Concert ni matamasha endelevu ya kumtolea Mungu  dhabihu za sifa yanayoandaliwa na watu wa mungu bila ya kujali jinsia,umri,rangi,kabila, wala Imani.

Kusudi la Sacrifice Of Praise Africa Concert ni kumtolea BWANA dhabihu za sifa na kuhudumia watu kutoka pande zote kwa nyimbo za kusifu na kuabudu, sala, pamoja na maombi, na shuhuda mbalimbali kupita kwaya na uimbaji wa mtu mmoja mmoja.

Pia kupitia matamasha haya wamekusudia kuibuwa vipaji vya wasanii wa nyimbo za injili ambao bado hajatoka wa kufamika katika muziki wa injili kwa kupatiwa mafunzo  ya kitaalamu ya muziki na uimbaji.

Kwa lengo la kuwasimamia katika kazi wasanii wa nyimbo za injili, kuandaa matamasha ya nyimbo za injili, mafunzo ya ufundi mitambo, mafunzo ya muziki na sauti, na pia kutoa mafunzo ya muziki wa live na kurekodi.

Malengo ya Sacrifice Of Praise Africa Concert kwa mwaka huu wa 2015 kabla ya uchaguzi ni kufanya ibada hizi (matamasha haya) na maombi ya amani kwa taifa la Tanzania.Kwa mwaka huu Sacrifice Of Praise Africa Concert inataraji kufika katika mikoa mitano hapa Tanzania; Arusha, Morogoro, Dodoma, Mbeya, na Dar es Salaam

Kwa dhumuni la kuifikia Africa nzima kwa uinjilisti wa nyimbo na kuunganisha mtandao wa wasanii wa nyimbo za injili Afrika nzima.

Ungana nasi katika tukio zima la Sacrifice Of Praise Africa Concert Season 2 Tanga ambayo ilifanyika katika kanisa la E.A.G.T mikanjuni kuanza saa nane mchana ambapo dhabihu za sifa zilianza kushuka.


 Selestina Nyangusi
 Hatimaye Dezzydery akimkaribisha  MC King Chavala


 Shela Mnyinyi katika uimbaji wake akamsifu Mungu kwa nyimbo ya kiasili


 Na huyu ni Edna Kuja kutoka Dar es salaam 

 Mchungaji wa kanisa la E.A.G.T Mikanjuni - Josephine 

Katika kuwekwa wakfu Sacrifice Of Praise Africa msimu wa pili Tanga
 Wimbaji Christina Msengu katika uimbaji wake
  Na huyu ni Hellen Kijazi


 katika upigaji wa saxophone Mise Anaeli kutoka Dar es salaam 
 Daniel Manimba, Mratibu - Sacrifice Of Praise Africa Concert


 Dezzyderry, Mratibu - Sacrifice Of Praise Africa Concert

Mwalimu Emmanuel Mkawaya 
 Mzee Ambaye aliguswa na kuitaji kutoa mchango wake wa kifedha katika kufanikisha matamasha endelevu ya Sacrifice Of Praise Africa Concert na sasa ni Sacrifice Of Praise Africa Concert Mass Choir
 uwepo wa Bwana Yesu ukishuka katika Dhabihu za sifa


 Katika uwepo wake

 Ni katika ugawaji wa zawadi/vyeti ambayo vilionyesha juu ya kushiriki katika Sacrifice Of Praise Africa Concert msimu wa pili. 


 Upigaji wa picha za pamoja watu wakiwa na furaha kubwa mmno kukamilisha kumpa Mungu dhabihu za sifa 


Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.