KWA TAARIFA YAKO: MUIMBAJI WA BONGO FLEVA ALIYENG'ANG'ANA NA WOKOVU ZAIDI YA MIAKA 7 SASA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


K-Basil akiwa katika kora ya kichungaji

KWA TAARIFA YAKO siku ya leo bado tunaendelea kukujuza kuhusu watumishi wa Mungu nchini, wiki iliyopita tulikuwa nchini Nigeria tukakujuza kuhusu nabii TB Joshua na mama askofu Upendo Nkone wiki ya jana yake kama hukusoma BONYEZA HAPA. Leo tunakujuza kuhusu mmoja wa waimbaji aliyevuma wakati huo akiwa anaimba nyimbo zisizo za kumsifu Mungu kisha kukata shauri na kumpokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Mwimbaji huyu tumewahi kuandika habari zake siku zilizopita ila kwakuwa miaka inazidi kusonga basi hapana shaka kukujulisha hili.

KWA TAARIFA YAKO watu wengi wamekuwa hawaamini pale wanaposikia waimbaji wa muziki wa bongo fleva ama muziki wa nje ya kanisa wanapotangaza kuwa wameokoka kutokana na jinsi wanavyoonekana kwa jamii na majina yao yalivyo makubwa katika muziki wao. Wengi wao hudhani kwamba watu hao hudanganya umma ama wanatangaza hivyo kwaajili ya kupata kitu fulani na huwapa muda kwamba lazima baada ya kipindi hicho watarejea katika mambo yao ya zamani.


K-Basil mkono wa kuume akiwa na mmoja wa rafiki zake na mtumishi katika kanisa la Ufufuo na Uzima.
KWA TAARIFA YAKO hapana shaka unamkumbuka mwanamuziki Basil Kashumba au jina alikuwa akifahamika zaidi kama K-Basil aliyetamba na nyimbo kama Bahati haiji mara mbili pamoja na Riziki ambao alimshirikisha mwimbaji Stara Thomas ambaye naye alitangaza kuokoka kabla hajarejea kuimba muziki huo kwa mara nyingine. KWA TAARIFA YAKO K-Basil ni mchungaji na bado anasonga mbele na wokovu wake tangu atangaze kuokoka miaka takribani saba iliyopita. 

KWA TAARIFA YAKO mwimbaji huyu mkazi wa Tabata Segerea jijini Dar es salaam, ni mchungaji na muumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es salaam chini ya kiongozi na muasisi wa kanisa hilo Askofu Josephat Gwajima. Aidha si kwamba Basil ameacha uimbaji la hasha mara baada ya kuokoka aliendelea na kipaji chake cha uimbaji kwa kumwimbia Mungu wake.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa wiki hii kama ulikuwa hujui ni kwamba Kashumba Basil au K-Basil bado amesimama kidete kwenye wokovu kwahiyo kuwa na imani na watu unaodhani hawawezi kuokoka na kusimama, kikubwa endelea kuwaombea. Vinginevyo tukutane wiki ijayo….
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.