KWA TAARIFA YAKO: MWIGIZAJI MWINGINE WA MAISHA YA YESU ANAVYOPAMBANA NA MAJARIBU

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

KWA TAARIFA YAKO kama hujui ni kwamba mwigizaji wa majukwaani na sehemu za wazi wa igizo la maisha ya Yesu anayefanana sana na mwigizaji halisi wa filamu ya Yesu iliyoigizwa na mkongwe Brian Deacon, kijana James Burke Dunsmore ambaye pia ni mwingereza kama ilivyo kwa Brian, ameweka wazi majaribu anayokutana nayo toka ameanza kuigiza igizo la maisha ya Yesu majukwaani.

KWA TAARIFA YAKO James ambaye ni mkazi wa jijini London alimaliza elimu yake ya juu katika mambo ya sayansi za majukwaani katika chuo kikuu cha Middlesex kilichopo jijini London, wakati huo akiwa aamini mambo ya Mungu na Biblia kwa ujumla. James anasema siku moja kupitia mabishano na wanafunzi wenzake kuhusiana na mambo ya dini na kwamba alipinga kila alichoambiwa na mwenzake akiwa amejiwekea lengo la kutoshindwa kwenye mabishano yao. Lakini anasema kutokana na mabisaho hayo ndipo alipogundua namna dini ilivyoshika mizizi Uingereza na kwamba kila alipotoka kwenye mazungumzo na wenzake basi mazungumzo yao yatabaki akilini mwake mda wote.

Waigizaji wa nafasi ya askari waliomwangamiza Yesu wakiwa katika viwanja vya Trafalgar square London 2012


KWA TAARIFA YAKO kwa kifupi ni kwamba James aliamua kumfuata Kristo kwasababu masomo aliyokuwa akiyasomea siku moja akapangiwa kuigiza sehemu ya Yesu kitu ambacho hakupingana nacho mpaka leo hii. Lakini kikubwa kutoka kwa mwigizaji huyo nyota mwenye miaka 40 na kwasasa, majaribu anayokutana nayo kutoka kwa watu mbalimbali wakiwepo wasioamini uwepo wa Mungu ni pamoja na kuletewa chupa zilizojaa maji na kutakiwa kuzibadilisha na kuwa mvinyo, pamoja na miujiza mingine ambayo Yesu aliitenda kama Biblia isemavyo.

KWA TAARIFA YAKO James ameanza kuigiza nafasi ya Yesu akiwa na miaka 16 mpaka sasa akiwa tayari ameshiriki kwenye maonyesho tofauti zaidi ya 57 pamoja na kuandaa na kuhariri miongozo ama scripts kwa vitabu vingine vya injili zaidi ya 32, na kila inapotokea kuigiza nafasi ya Yesu huchaguliwa yeye kwani pia ameshiriki kuigiza katika filamu nyingine iliyoandaliwa nchini Afrika ya kusini. Sambamba na kuigiza sauti ya Yesu katika igizo la redioni na kwenye runinga. Pia ameshiriki kuzungumza zaidi ya mara 40 kwa siku na wanafunzi katika shule akiwaelezea umuhimu wa neno la Mungu na si maneno ya kawaida kama wanafunzi hao wayasomavyo. Lakini pia mwigizaji huyu alishatembelea nchini Kenya.

Ambwene akiwa na James mara baada ya kumaliza kuigiza viwanja vya Trafalgar square London 2012


KWA TAARIFA YAKO kipaji chake cha uigizaji kiliboreshwa zaidi kupitia shirika la kidini la Wintershall ambao huandaa maonyesho ya wazi ya igizo la Yesu ambalo kwa wakazi wa jiji la London hujionea bure kila siku za Ijumaa kuu katika eneo la wazi la Trafalgar square lililopo katikati ya jiji hilo.  Pamoja na majaribu anayokumbana nayo mwigizaji huyo lakini pia kuna shuhuda kutoka kwa watu ambao amekuwa akikutana nao ambao humwambia namna uigizaji wake ulivyoweza kuwakutanisha na Mungu huku wengine ambao hawaamini neno la Mungu kujikuta wakiangusha kilio kizito wanapomuona anaigiza kwa hisia. 

James akiwa anaigiza kipande cha mwisho cha kufufuka kwa Yesu viwanja vya Trafalgar square London 2012


Unaweza kujionea picha mbalimbali zilizonaswa na GK wakati James akiigiza ili kuziona BONYEZA HAPA na HAPA 

Ama kusoma na kujua historia ya mwigizaji wa filamu ya maisha ya Yesu, BONYEZA HAPA


Mdau wetu hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo japo kwa ufupi, vinginevyo tukutane wiki ijayo…
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.