KWA TAARIFA YAKO: SAFARI YA TB JOSHUA HADI KUTOKEWA NA MUNGU KWA AJILI YA KAZI

TB Joshua.
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Ni wananchi wengi Tanzania na hata Afrika Mashariki kwa ujumla wanafahamu na kutambua uwepo wa mtumishi wa Mungu kutoka Nigeria, TB Joshua. Nabii huyu ambaye si mgeni kwenye runinga za wana Afrika Mashariki, amejizolea umaarufu kutokana na mahubiri yake pamoja na unabii ambao huwa anatoa na hatimaye watu kuwa mashuhuda baada ya kitambo kupita. KWA TAARIFA YAKO, pamoja na yote hayo, si wote wanaofahamu aliyopitia. Leo tutakupa japo kwa uchache.

Jambo la kwanza inaelezwa kwamba TB Joshua alikuwa tumboni kwa mama yake kwa kipindi cha miezi kumi na tano, na dabo alizaliwa mwenye nguvu bila matatizo yoyote.

Kuzaliwa kwake kwenye maisha kwenye familia maskini kulimfanya apitie na kujifunza mengi sana hadi kufika sasa, ambapo KWA TAARIFA YAKO alipoanza tu shule ya sekondari, ilimpasa kuachana na shule akiwa mwaka wa kwanza tu na hivyo kuendelea kutafuta riziki kuendeleza maisha. Lakini akiwa shule ya msingi, pamoja na udogo wake aliokuwa nao alikuwa ndiye kiongozi wa usharika wa wanafunzi wenzake. Na KWA TAARIFA YAKO alikuwa akifahamika kwa jina mchungaji mdogo (Small pastor)


SCOAN, ama kwa marefu yake Synagogue Church for All Nations, KWA TAARIFA YAKO iliazna kwa watu 8, lakini hadi sasa makumi elfu ya watu humimina na kubarikiwa sawasawa na haja ya mioyo yao.

Yote kwa yote ni namna mtumishi huyu alivyopokea huduma hii akiwa kwenye maono kwa siku tatu mfululizo, ambapo KWA TAARIFA YAKO aliota anakabidhiwa Biblia ambayo iliingia moyoni mwake. Kuambatana na hayo ni pale alipumuona Yesu akiambatana na mitume wengiine, ambapo kubwa zaidi ni uwepo wa mtu ambaye hakumtambua uso wake kwa namna ambavyo alikuwa anang'aa hadi akashindwa kumuona. Lakini aligundua kuwa ndiye Mungu huyo aliyekuwa akimuongelesha kwa habari ya huduma yake.

KWA TAARIFA YAKO kati ya mitume na wanafunzi na manabii aliowaona ni pamoja na Petro, Paulo, Musa, Eliya, na wengineo ambapo majina yao yalikuwa yameandikwa vifuani mwao.

"Mimi ni Mungu, na ninakusimika ukaifanye kazi hii ya baba wa Mbinguni" ni maneno ambayo TB Joshua aliambiwa na Mungu na kisha KWA TAARIFA YAKO kukabishiwa msalaba mdogo na Biiblia kubwa.

Hata sasa, bado kazi ya Mungu inasongeshwa huku mataifa yakifahamu vema kile kinachoendelea kutokea mashariki ya mbali. NI mengi ambayo tunaweza kuandika kuhusin mhubiri huyu, lakini kwa leo basi tuishie hapa.

Hiyo ndo KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.