KWA TAARIFA YAKO: UPENDO NKONE ALIVYOSITISHA IBADA KANISANI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Upendo kone akiimba na Christina Matai Naioth Gospel Assembly hivi karibuni.
Kati ya waimbaji ambao wamekuwa wakigusa mioyo ya waumini wa Kikristo basi huwezi kuacha kumtaja mwanamama Upendo Nkone. mama huyu ambaye familia yao imekuwa ya wachungaji, anatambulika kama Mama Askofu Mbeyela. Kati ya upekee alionao ni kwamba mara nyingi huwa anazungumza kabla ya kuanza kuimba. Na hii imekuwa ikiwabariki mno waumini wanapokuwa ibadani.

Moja kati ya ibada ambayo alihudumu na kubariki mamia ya waumini kupitiliza ni kanisa lake la nyumbani Naioth Gospel Assembly Mabibo External kwa Askofu David Mwasota. KWA TAARIFA YAKO mapema mwaka huu baada ya wahudumu kadhaa kusifu na kuabudu, ilifika zamu ya Upendo, ambapo mara baada ya yeye kushika kipaza sauti, basi ibada iliishia kuahirishwa hata kabla Mchungaji kuhubiri.

Tukio lenyewe likiwa halielezeki, lilipelekea waumini kububujikwa na kuzama rohoni katiba kumuabudu Mungu na kisha kila mmoja akazama kwenye maombi, jambo ambalo ni nadra kutokea kulingana na ratiba za ibada zilivyo. KWA TAARIFA YAKO siku hiyo kila mtu alitoka mwepesi ibadani, kwani maombi yaliyofuatia hapo hayakuwa ya kawaida, uwepo wa Mungu ulijidhihiri.

Pata wimbo mmojawapo - Nakushukuru

Pamoja na uwezo mkubwa mno alionao mama mchungaji huyu, pia amekuwa wa baraka sana kila anenapo jambo, ambapo KWA TAARIFA YAKO kati ya matamasha aliyowahi kufanya kitu cha kipekee pia tofauti na kuimba tu kama ilivyo ada kwa wengine, ni kwenye tamasha la Upendo kwa Mama ambalo lilifanyika kwa mara ya kwanza jijini Arusha, mwanamama Upendo Nkone alitumia takribani nusu saa kushuhudia na kueleza namna gani Mungu amemvusha katika hatua ngumu alizopitia, na kisha kufanya maombi na watu walijitokeza kwenye tamasha hilo na kisha kushuka. Ambapo alikuja kurudi baadae jukwaani na kuimba nyimbo mbili ambazo ziligusa maelfu ya umati uliojazana kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume.

Maombi baada ya kuimba mkoani Shinyanga
KWA TAARIFA YAKO tukio kama hilo pia amewahi kulifanya kwenye tamasha la pasaka mkoani Shinyanga kwenye Uwanja wa Kambarage, ambapo pamoja na kuhudumu kwa njia ya uimbaji, aliposhuka jukwaani alipata wasaa wa kufanya maombi na wenye uhitaji. Kuna mambo ya kujifunza hapa tofauti na kuimba na kuruka sarakasi kisha kupigiwa makofi.

Lakini pamoja na yote kuna mdau mmoja hupenda nyimbo za Upendo Nkone, naye si mwingine bali ni mume wake, Askofu John Mbeleya. KWA TAARIFA YAKO wimbo ambao unamgusa kuliko zote ni wa "Yesu Nakuja Kwako". Wimbo huu Askofu Mbeyela huuita kwamba ni wimbo wake.

Bwana na Bibi Mbeyela
Pamoja na hayo, kama ulikuwa hujui, kwenye album yake ya Uniongoze Yesu - Upendo ana nyimbo ambazo hupenda sana, mojawapo ambayo hakika ikiwa inaimbwa sehemu hata yeye mwenyewe hawezi kutulia ni "Muombe Mungu". Na hii ndo KWA TAARIFA YAKO kwa wiki hii, vinginevyo tukutane wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.