MITO YA BARAKA ILIVYOFURIKA NYIMBO ZA SIFA JUMAPILI ILIYOPITA

Jumapili iliyopita June 7 lilifanyika tamasha la kusifu na kuabudu katika kanisa la EAGT Mito ya Baraka lilipo maeneo ya Jangwani karibu na klabu ya Yanga jijini Dar es salaam, Kanisa ambalo linaongozwa na Askofu Dkt Bruno Mwakibolwa.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na watu wengi kiasi cha wengine kusimama ambao watu walianza kufika tangu ibada ya pili kanisani hapo. Mnamo majira ya saa tisa tamasha hilo lilianza kwa kikundi cha kusifu na kuabudu cha kanisani hapo kuanza kwa kufungua, na baada ya hapo waimbaji wengine walianza kumsifu Mungu kama walivyotangazwa kwenye Matangazo.
Waimbaji ambao walihudumu ni Kiza Blessing,  Steven John ambaye ni mlemavu wa macho, Naomi Anangisye, Deborah Mwaisabila, Christina Mbilinyi, Oscar Nyerere aliyekuwa akiigiza sauti za viongozi mbalimbali wa kitaifa, Rev Ambele Chapanyota, Mchungaji Nicodem Mwahangila,  Martha na Beatrice Mwaipaja na Emmanuel Mgaya au Masanja Mkandamizaji.
Pamoja na hao wote kuhudumu, wawili walishindwa kutokea, ambao ni Christopher Mwahangila na Martha Baraka, japo hilo halikukwamisha tukio zima kusonga. Kanisa la Mito ya Baraka hufanya matamasha ya kusifu na kuabudu kila jumapili ya kwanza ya mweni hivyo tamasha lingine linatarajiwa kufanyika July 5.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.