MWIGIZAJI NYOTA AUNGA MKONO WAOKA KEKI WALIOKATAA OMBI LA KEKI YA WAPENZI WA JINSIA MOJA

Nembo ambayo si rasmi ya ndoa ya jinsia moja inayofahamiaka kama Bert na Ernie ©news.com.au
Mmoja wa waigizaji nyota walioigiza filamu ya X-Men pamoja na Star Trek aitwaye Patrick Stewart, ameunga mkono uamuzi wa watengeneza keki wa Kikristo wa nchi ya Ireland ya kaskazini ambao walikutwa na hatia ya ubaguzi na kulipishwa faini, kwa uamuzi wao wa kukataa kutengeneza keki yenye ujumbe wa kuunga mkono ndoa za jinsia moja wakifuata imani ya dini yao.

Akizungumza wakati wa mahojiano na BBC kupitia kipindi cha "Newsnight" na video ya kipindi hicho kutolewa alhamisi iliyopita, mwigizaji huyo ameonyesha kuunga mkono uamuzi wa kampuni hiyo ya kuoka vitafunwa iliyoko mji wa Belfast, iitwayo Ashers Bakery Company mali ya Colin na Karen McArthur akisema kwamba waokaji hao walikataa si kwamba walipinga wapenzi hao wajinsia moja, ama walikuwa wanasherehekea aina ya ndoa ama makubaliano kati yao, la hasha bali maneno waliyoambiwa waweke kwenye keki kwakuwa yalikuwa kinyume na imani yao. "Ningependa kuwaunga mkono na msimamo wao, hiyo ni haki yao kuhusiana na imani, sitafanya hivyo, ila najisikia vibaya kwakuwa msimamo wao umewagharimu pesa" alisema Stewart

Mwanaharakati Gareth Lee alitoa oda ya kutengenezewa keki hiyo kwa tukio la faragha katika kusherehekea siku ya kimataifa ya kupinga vitendo vya unyasasaji kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ambapo mara ya kwanza muokaji alikubali kutengeneza keki hiyo kwa mujibu wa mtandao wa news.com.au ambao ulidai muokaji alikataa oda hiyo siku mbili baadae. Aidha taarifa zinadai keki hiyo ilikuwa akabidhiwe meya wa Ireland kaskazini ambaye alikuwa wa kwanza kwa upande wa viongozi kutangaza kwamba yeye ni shoga.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.