OMBA YESU ANASIKIA YA UPENDO NKONE YAZINDULIWA RASMI NCHINI MAREKANI

Upendo Nkone katikati wakati wa maombi yaliyoongozwa na mchungaji Donis Nkone na mkewe  kuzindua album hiyo.©Donis Nkone

Nyota wa muziki wa injili nchini mwanamama Upendo Nkone ama kwa jina lingine mke wa Askofu Mbeyela, aliweka wakfu album yake mpya ya tano aliyoipa jina la 'Omba Yesu Anasikia' katika ibada iliyofanyika huko nchini Marekani.

Upendo ambaye yupo ziarani nchini Marekani alizindua album yake hiyo katika kanisa la kiswahili la All Nations BreakThrough Church (ANBC) lililopo huko Columbus Ohio linaloongozwa na mchungaji Donis Nkone ambaye ni kaka wa mwimbaji huyo ambaye matoleo yake manne yaliyopita bado yameendelea kuwabarikia maelfu ya watu waliopata kununua kazi zake, hasa kutokana na jumbe, muziki na sauti zinazopatikana katika nyimbo zake. Album hiyo inaanza kupatikana nchini wiki hii.

Maombi ya uzinduzi
Baadhi ya waumini wakimsikiliza mwanamama Upendo Nkone Mbeyela wakati akiimba (hayupo pichani)©Donis Nkone.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.