SHANGWE ZA GK : HATUA ZA KUCHUKUA KUMPATA MCHUMBA MZURI - MCHUNGAJI MITIMINGIKWA VIJANA WANAOTAFUTA MCHUMBA!
HATUA ZA KUCHUKUA KUMPATA MCHUMBA MZURI - MCHUNGAJI PETER MITIMINGI

1. Usifanye haraka kutamka neno lolote kwa mtu unayetaka awe mchumba wako hata kama utakuwa umehakikisha ni Mungu kakuonyesha.
2. Mchumba mzuri atakaye kufaa maishani mwako ni yule ambaye UTAMCHUMBIA KABLA YA KUMCHUMBIA.
3. Baada ya kukamilisha hatua ya pili ndipo sasa hatua ya tatu Onyesha dalili za kumpenda bila kumtamikia kuwa unampenda wala unania ya kumchumbia.
4.Ukisha thibitisha na kujiridhisha ndipo sasa hapa katika hatua ya nne ndio unaweza kutamka neno sasa.
2. MCHUMBA MZURI ATAKAYE KUFAA MAISHANI MWAKO NI YULE AMBAYE UTAMCHUMBIA KABLA YA KUMCHUMBIA.
Nimeamua kutoa ufafanuzi wa hii pointi hasa kwa vijana wa kiume wanaotaka kuchumbia.
Kuchumbia kabla ya kuchumbia inamaanisha kwamba unapokuwa umemuona msichana ambaye unadhani umevutiwa naye ili labda aweze kuwa mke wako siku za usoni, kabla hujamtamkia waka kuonyesha dalili zozote unapanswa uanze kufanya uchunguzi wa awali kwa kutokea mbali bila hata yeye kuweza kujua au kugundua kuwa una mchunguza wala una nia nae yoyote. Katika wakati huu anakuwa mchumba wako wa kimoyomoyo bila hata kumshirikisha rafiki yako wala rafiki yake yeyote ni wewe tu na Mungu ndio mnajua wazo lililopo moyoni.
Baada ya kujiridhisha kwa uchunguzi wa hatua za awali sasa unaongeza gia nyingine unaonyesha dalili tu za "interest" bila kutamka neno lolote la kujicommit hii itakuwa ni hatua ya 3 ya uchunguzi kabla ya kuingia hatua ya 4 ambayo ni kumtamkia.

NAAMINI MPAKA HAPO NITAKUWA NIMEWATAFUNIA KABISA HAPO SASA KAZI NI KUMEZA TU!

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.