SOMO: JICHO LAKO LIKIKUKOSESHA LING’OE ULITUPE MBALI NAWE

Mchungaji Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Imeandikwa;

” Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum” Mathayo 5:29

Mtu mmoja alisema sasa ikiwa jicho langu limenikosesha,nikiling’oa si nitapata maumivu sana. Maana jicho linavyoumaa we! Alafu ndio uniambie niling’oe usifanye mchezo wewe,litaumaje!!!

Akaongeza kusema, ”… mimi nafikiri sheria ya namna hii,bhana haiwezekani,andiko limekosewa hili… sababu maumivu yake ni makubwa ati kung’oa jicho…” Hayo yalikuwa maneno ya mtu mmoja.

Mtu huyu hakujua maana halisi ya kungoa jicho linalokukosesha. Na hata hivyo,nikagundua kwamba wengi tunaelewa kama mtu huyo alivyokuwa akielewa kwa mfano wa jicho. Kumbe jicho linalozungumziwa hapo halikuwa na maana ya jicho kama jicho la kibinadamu.

Labda tuangalie maana halisi ya jicho kwa mfano huu.

Mtu mmoja aliyekuwa ameajiliwa katika kazi moja nzuri yenye kipato kizuri hapa hapa jijini Dar.Mara baada ya miezi michache kama miezi mitatu hivi,boss wake wa kike akampromoti. Katika miezi hiyo hiyo michache yule boss akamwongezea marupu rupu yasiyostahili maana kama kuongezewa basi walistahili wale waliokuwepo kabla yake.

Lakini kumbe boss alikuwa na malengo mabaya ya kumtaka kimapenzi. Huyu mwajiliwa alipoona hivyo,akaamua kuacha kazi kwa sababu alimkimbia boss wake mwenye kumtaka. Ni kama vile Yusufu alipomkimbia mke wa Potifa aliyemtaka alale naye ( Mwanzo 39:6-12 )

Kumbuka ajira yake (huyu mtu) ilikuwa inatija sana kumsaidia yeye pamoja na familia. Hivyo aliona ni afadhali sana kukosa ile kazi ambayo ilikuwa ndio taa ya maisha yake kuliko kumkosa Mungu na kuuokosa ufalme wa mbinguni pia. Kama mtu huyu angelikubali kutembea katika safari yake ya wokovu pamoja na ile ajira yake yenye uchafu ndani yake,basi ni dhahili kabisa angeliweza kuingia motoni pomoja na ajira yake.Kazi ya mtu huyu imefananishwa na jicho lake. Ambapo yeye aliona ni bora apoteze kwa ajili ya Kristo Yesu. ( Wafilipi 3:7-8 )

Jicho ni kiungo chenye kuleta mawasiliano ya kuona. Ni dhahili kabisa bila jicho mtu hawezi kuona. Hivyo hata matamanio yetu sisi wanadamu yanaanzia kwanza katika macho maana ndipo kwenye kuona.

Hivyo basi,chochote kile chenye kukuonesha au kuwa kisababishi cha kutenda jambo lolote lile, chaweza kufananishwa na jicho. Inawezekana rafiki yako akafanana na jicho kwako,maana wapo watu wenye kuongozwa na kuoneshwa vitu na marafiki zao. Sasa biblia inasema kuwa jicho lako likikukosesha ling’oe yaani ni afadhali sana ujitenge na huyo rafiki mwenye kukukosesha.

▪ Ni afadhali hata kuacha kazi fulani ambayo kwa hiyo ungemkosa Mungu wako.Kazi ni tamu,lakini kumbuka ni ya kutambo tu,utakufa na kuiacha.

Ifike wakati wa kuyatupa yale yote mabaya hata kama kwa nje yanapendeza. Yapo mambo ambayo unayafanya wewe mwenyewe tena kwa siri kubwa,mambo hayo kwa nje yanaonekana ni mazuri kiasi kwamba hata watu wanakusifia kwa hayo,lakini kwa hayo ndio yanayokuingiza Jehanum.

Mfano; Yupo mtu ambaye ana mahusiano ya kimapenzi na mume wa mtu ambaye kwa huyo mume hufaidi na uvalishwa vizuri. Mwanamke huyu,hupewa sifa na jamii jinsi anavyopendeza kwa muonekano wake wa nje lakini jamii yake ya karibu hawafahamu mafanikio yake yanatoka wapi isipokuwa yeye mwenyewe. Sasa huyu mume wa mtu anamkosesha mbingu huyu mwanamke.

Ni afadhali sana umng’oe na kumtupa huyu mwanamume pasipo kuangalia anakupa nini,kuliko kwenda naye motoni. Na kwa mwanaume naye ni vivyo hivyo,itakufaa nini kuonekana nadhifu machoni pa watu na kumbe lipo jicho linalokukosesha na kukufanya uingie Jehenum?

▪ Kwa huduma ya maombi na maombezi,nipigie 0655111149.

Mchungaji Gasper Madumla.

Beroya bible fellowship church ( Kimara,Dar-Tanzania )

UBARIKIWE.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.