SOMO: MAKUSUDI YA UTANDAWAZI KWA VIJANA - MCHUNGAJI MITIMINGI


Pata dondoo ya somo hili la utandawazi kwa vijana kama lilivyofundishwa na mchungaji Peter Mitimingi mkurugenzi wa huduma ya sauti ya matumaini ama VHM katika semina ya vijana iliyofanyika kanisa la Kilutheri usharika wa Ubungo jijini Dar es salaam.

MAKUSUDI YA UTANDAWAZI KWA VIJANA!

1. Utandawazi ulikusudiwa kujenga na kumrahisishia mwanandamu katika shughuli zake za kila siku.
2. Utandawazi ulilenga kumuwezesha mtu kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi na kwa urahisi.
3. Shetani amejiingiza katika utandawazi huo na kuutumia kubomoa badala ya kujenga.
4. Walengwa wakubwa katika utandawazi huu ni vijana.
5. Shetani anawatafuta vijana awatumikishe lakini Mungu pia anawatafuta vijana aweze kuwatumia.
• Ni vijana wanagapi wapo tayari kutumikishwa na shetani?
• Ni vijana wangapi wapo tayari kutumiwa na Mungu?

UTANDAWAZI NI KISU!
CHANGAMOTO ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

• Teknolojia ninaweza kuifananisha na kisu kikali.

• kisu ni kifaa ambacho kila familia inakihitaji kwajili ya kusaidia kurahisisha shughuli zetu mbalimbali.
• Kuna baadhi ya shughuli kama zikikosa kisu basi zinaweza kuwa ngumu sana kutekelezeka ni mpaka kisu kiwepo Mfano kuchinjia Ngombe, kukatakata nyama n.k
• Kisu hicho hicho ambacho kinatusaidia kufanya mambo mezuri kina uwezo wa kumdhuru mtu na kutoa uhai wa mtu.
• Kwahiyo inategemea sana matumizi ya hicho kisu. Kinaweza tumika vizuri kikasaidia au kinaweza tumika vibaya kikaleta uharibifu.
• Ndivyo ilivyo teknolojia inategemea sana matumizi yake kwa mhusika ikitumika vizuri itajenga na kumsaidia kijana lakini teknolojia hiyo hiyo ikitumika vibaya itaweza kuleta uharibifu katika maisha ya kijana.
CHANGAMOTO YA MTANDAO WA FACEBOOK KWA VIJANA

Anza kwa Kujiuliza Maswali Haya:
1. Kwanini upo facebook?
Orodhesha sababu zote zinazokufanya uwepo Facebook.
Kisha tathmini kama sababu hizo kama ni za msingi.
2. Nini kinakunufaisha na facebook?
Orodhesha manufaa yote unayoyapata katika facebook.
3. Kuna utofauti gani unapokuwa na facebook na unapokuwa huna facebook.
Orodhesha faida zote au manufaaa yote unayoyapata kupitia Facebook.
Kisha Orodhesha hasara au masumbufu unayoyapata kwa wewe kuwepo facebook.
Linganisha kama ukiona hasara ni nyingi kuliko faida basi nakushauri utoke na uachane na facebook maana itakakokufikisha huenda kusiwe kuzuri.
4. Unachukua tahadhari gani kwa kupambana na waharibifu na uharibifu uliopo ndani ya facebook.
Katika facebook kuna watu na mambo yasiyofaa pia.
Umejiwekea mkakati gani kukabiliana na mambo yasiyofaa yaliyopo facebook?
Pamoja na baadhi ya mambo mazuri yaliyopo facebook kuna mambo megi yasiyo mazuri katika mtandao wa facebook ambayo kama kijana hatakuwa makini basi facebook inaweza kumletea uharibifu badala ya mema.
Tito 2:11 - 12
11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
CHANGAMOTO ZA TELEVISION – RUNINGA KATIKA UTANDAWAZI

• Luninga ni chombo kizuri ambacho kwa upande fulani kinatupa habari za mammbo mbalimbali yanayoendelea duniani kote.
• Kwa upande wa pili luninga kimekuwa ni moja ya chombo ambacho shetani pia anakitumia kwa kazi sana katika kusafirisha na kufikisha mambo yake mabaya kwa jamii na hasa vijana.
• Kupitia chombo hiki vijana wameweza kuona mambo mabaya ambayo kwa sehemu kubwa yanaharibu maisha na maadili ya vijana wetu wengi katika siku ya leo.
Utafiti wa Kitaalam:
Mwandishi mmoja “Mark Cover” katika kitabu chake cha faith “Begins at Home” amefanya utafiti na kusema kwa mtoto TV inachangia asilimia moja tu, 1% ya mambo mema ambayo mtoto anaweza kujifunza kutoka katika Tv. 99% ya mambo ambayo mtoto tajifunza kutoka katika Tv yatakuwa ni ya kumbomoa na kuharibu maadili mema aliyoyapata.
Baadhi ya Mambo Yasiyomjenga Kijana Kutoka katika Luninga (Tv)
• Miziki ya kidunia
• Miziki inayoonyesha watu wakiwa katika mavazi ya utupu au nusu utupu
• Filamu zinazozungumzia mapenzi.
• Channel za Ngono
• Program zinazo mhamasisha na kumsisimua kijana kuingia dhambini.
Ushauri kwa Kijana Kuhusu Utandawazi wa Luninga (Tv)
Ni vema vijana wakajifunza kuchagua ni program gani za kuangalia na nini cha kukiepuka kukiangalia katika Luninga zao ili kulinda maadili mema na kuendelea kubakia salama.
Kumbuka kwamba Imani chanzo chake ni kusikia.
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

NEEMA 8 ZILIZOFUNULIWA KUMSAIDIA KIJANA
SEMINA YA VIJANA KKKT UBUNGO
1. Zamani tulifanya kwa ujinga sasa neema imefunuliwa
2. Mungu ameifunua neema ili kuwaokoa vijana wasiendelee kuangamia
3. Neema hii inatufundisha vijana kukataa ubaya na mambo yote mabaya.
4. Neema hii inatufundisha vijana kukataa TAMAA za kidunia.
5. Neema hii inatutaka vijana tupate kuishi kwa KIASI
6. Neema hii inatutaka vijana tupate kuishi kwa HAKI
7. Neema hii inatutaka vijana tupate kuishi kwa UTAUA katika ulimwengu huu wa sasa uliojaa maofu.
8. Kuishi maisha safi ndani ya jalala.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.