SOMO: NAMNA YA KUTAMBUA HABARI/TAARIFA YA UONGO KWENYE MAISHA YAKO

Na Faraja Mndeme,
GK Contributor.

1. JE HABARI/TAARIFA INAYOELEZEWA INAPENDELEA?
Mara nyingi tumejikuta tunaingia kwenye mkanganyiko wa kushindwa kuelewa  kwamba taarifa/habari fulani ni sahihi au hapana. Moja ya njia rahisi inayoweza kukusaidia kutambua habari hiyo inaweza kuwa sahihi au hapana ni kuangalia je inapendelea upande wowote. Ukiona habari inapendelea upande wowote tambua habari hiyo ina walakini. Habari yoyote iliyo sahihi haipendelei upande mmoja na kuukandamiza mwingine. Habari/Taarifa sahihi huelezea uhalisia wa jambo bila kulalia Upande wowote. Lengo la taarifa/habari  ni kuwapa watu/jamii taarifa na sio kuonyesha upi ni upande sahahi. Wala pia lengo la habari/taarifa sio kutoa  hukumu bali ni kuifahamisha Jamii kwamba hiki ndicho kinachoendelea na jamii yenyewe ndio iamue kutoa hukumu.

2. JE UADILIFU WA MTOA TAARIFA/HABARI UKOJE?
Uadilifu kwenye swala la maisha ya mtu binafsi ni swala muhimu  sana kwenye utoaji wa taarifa/habari. Ni muhimu sana kujua uadilifu na maisha ya mtu au chombo ambacho kinakupa taarifa/habari fulani. Maisha ya mhabarishaji ni muhimu sana. Uadilifu ni swala ambalo ni la muhimu sana. Maana fikiria uadilifu wa mtu anayekupa habari/haueleweki na ukajikuta unazibeba tu taarifa hizo. Unaweza kujikuta unaingia kwenye matatizo na vyombo vya dola au unaweza kusababisha madhara kwenye jamii inayokuzunguka, ambapo haya mambo yangewezeka kuepukika. Jaribu kufikiria mtu anaeyekupa taarifa ana tabia ya uongo. Je unafikiri taarifa/habari anazokueleza zitakuwa za namna gani? Ni muhimu kupima uadilifu wa mtoa taarifa/habari ili kujua iwapo habari/taarifa upewayo ni ya ukweli au uongo.

3. JE HABARI/TAARIFA UNAYOPEWA INA UTHIBITISHO KIASI GANI?
Habari/Taarifa nyingi tunazopewa huwa hazina uthibitisho wa kutosha sababu  huwa hatuna muda wa kuzithibitisha. Habari/taarifa nyingi huwa ni za kusikia na kusoma tu huwa hatuna juhudi za makusudi za kuthibitisha kile tunachoambiwa. Epuka kubeba habari za kusikia na kuambiwa au kusoma mahali bila wewe mwenyewe kuwa na chanzo cha uthibitisho wa habari/taarifa husika. Taarifa/Habari unayoambiwa lazima unakuwa na chanzo chake  na unapopata chanzo cha habari/taarifa husika inakusaidia kuwa na uhakika wa kuthibitisha habari/taarifa husika. Watu wengi hutoa habari/taarifa zisizo sahihi huenda kwa sababu ya manufaa fulani wanayoweza kupata kutokana na taarifa husika bila kuangalia madhara wanayoweza kupata wapokeaji.

4. JE HABARI/TAARIFA HUSIKA  INA MANUFAA  GANI KWAKO?
Kuna habari/taarifa nyingine hata usipo zifahamu/kuzifahamu huwa hazina madhara yoyote. Ni muhimu kujiuliza kile unachotaka kupokea kina faida gani? Ulimwengu tunaoishi sasa una taarifa/habari nyingi sana - unaweza kushindwa ushike lipi na uache lipi. Hakikisha unapunguza kusikiliza na kusoma vitu visivyo na umuhimu ambapo vinajaza nafasi ambayo ulikuwa unapaswa kutumia kwenye mamabo mengine. Mambo ni mengi na hatuna muda wa kutosha wa kufanya kila jambo, imekupasa kuchagua na  kuweza kufanyia kazi habari/taarifa zenye umuhimu na faida kwenye maisha yako ya kila siku. Hakikisha unajenga uwezo wa kulinda, kutunza na  kukuza ubongo na akili yako kwa kusoma, kufwatilia habari zenye umuhimu na tija kwenye maisha yako ya kila siku. Habari zisizokuwa za kweli zinaweza kukuharibia mambo mbali mbali kwenye maisha yako ya kila siku.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.