SOMO: NGUVU YA TABIA - FARAJA MNDEME

Na Faraja Naftal Mndeme, 
GK Contributor.NGUVU YA TABIA Tabia ni mazoea yanayotokana na kurudiarudia hali,mwenendo au matendo ( Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la 3). Kila tabia unayoiona kwa mtu leo ni matokeo ya maamuzi mbali mbali yaliofanyika nyakati zilizopita,hakuna jambo ambalo linatokea kwenye maisha ya mwanadamu kwa sababu linatokea bila kuwa na chanzo fulani.Unapoona aina fulani ya tabia kwenye maisha ya mtu ni taarifa kwamba haya ndio maamuzi aliyoyafanya nyakati zilizopita.Hakuna tabia iliyopo kwa mtu ilitokea tu kama ajali.
Mara nyingi tumejikuta tumekuwa na mlundikano wa aina mbali mbali za tabia bila kujua wapi zilianzia na muda mwingine huku hatukujua namna ya maamuzi tulioyachukua kwamba yameathiri mfumo mzima wa tabia zetu. Kila jambo alifanyalao mwanadamu lina faida na hasara yake hakuna jambo ambalo halina faida na ambalo halina hasara hali kadhalika tabia ya mtu unayoiona leo inawezo wa kuibadilisha kuibadilisha kesho yake iwe njema au iwe mbaya. Kuna mambo mara nyingi kwenye maisha yetu huwa hatuyapi umuhimu kubwa kwa sababu huwa hatuoni matokeo yake na madhara yake papo kwa hapo ndio maana hatutumi muda mwingi kuwekeza kwenye mambo hayo.Ni muhimu kujifunza na kutambua kwamba kuna mambo ambayo ni muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku na imetupasa kujenga uwezo kila siku kwa kuwekeza ufahamu wa kutosha.Kuna Vitu ambavyo ukiviangalia kwa haraka haraka ni kama havina thamani lakini muda mwingine vina thamani kubwa kuliko fedha na dhahabu unazoziona. Moja ya jambo muhimu unalopaswa kutiliwa umanani na mkazo mkubwa ni namna unavyojenga tabia yako kwenye maisha yako ya kila siku.Tabia ni moja ya rasilimali muhimu kwenye maisha ya mwanadamu ambayo thamani yake ni kubwa kuliko fedha na dhahabu.Mara nyingi watu wengi tumetumia muda mwingi kuwekeza muda na rasilimali zetu kwenye mambo ambayo muda mwingine sio ya lazima huku tukisahau mambo ambayo ni ya muhimu kwa maisha yetu yajayo na kwa vizazi vyetu vijavyo. Zifwatazo ni Faida Chache za Kuwa na Tabia Njema. Tabia Njema ni Mtaji ,Mara nyingi huwa tunapoambiwa mtaji huwa tunafikiria kuhusu fedha lakini je ni kweli kwamba mtaji wa kweli ni fedha? Mara nyingi unapoenda kukopa kwa mtu au unapotaka msaada kwa mtu jambo la kwanza kabla haujapewa msaada wa jambo lolote huwa kinachoangaliwa ni aina ya tabia uliyo nayo.Fikira iwapo mtu ana taarifa kwamba una tabia ya wizi,utapeli na ulaghai alafu unaenda kwake kukopa unafikiri anaweza kukupatia fedha?la hasha maana tayarii tabia yako si njema.Huu ni mfano mdogo tu.Lakini imekupasa kutambua aina ya tabia ulio nayo leo ndio aina ya mataji ulio nao.Kuna mahali fedha inaweza isikupe nafasi lakini tabia inatakupa nafasi ya kuvuka na kupenya kwenye vipingamizi ambavyo fedha haikuweza kupenya. Tabia Njema ni Mlango wa Mafanikio yako yajayo,Mara nyingi hata unapoenda kuomba ajira kwenye ofisi mbali mbali moja ya uhakika wanaotaka kuupata ni aina ya tabia ulio nayo.Embu fikiria unapenda kuomba kazi wanagundua kwamba una tabia ya uvivu.Ji unafikiri unaweza kupata ajira unayohitaji? Tabia njema ni moja ya jambo ambalo likakuhakikishai kesho njema nay a uhakika.Tabia njema hukusaidia kupata rasilimali ambazo hapo mwanzo haukua na uwezo wa kuweza kuzipata.Tabia njema hukuakishia mafanikio ambayo wengine hawakuweza kuyafikiria na wala kuyawaza.Ni muhimu kuhakisha unawekeza kwenye ujenzi wa tabia njema maana ina kuhakikishia maisha yako bora yajayo. Tabia Njema husaidia kulinda kiwango cha mafaniko unayoyatarajia na uliyo nayo sasa.Ni rahisi sana kuweza kufikia kiwango cha juu cha mafanikio lakini ni ngumu sana kuweza kuendelea kubaki kwenye kiwango kile kile cha juu cha mafanikio ambayo umeyapata.Moja ya silaha muhimu ya kuweza kusaidia kuendelea kuwa mshindi zaidi ya pale ulipo leo ni namna unavyoweka juhudi zako kwenye ujenzi wa tabia njema.Mfano Mzuri kabla mtu hajapata mafanikio anakuwa mnyenyekevu na mwenje juhudi lakini akiwa amepata muonjo wa mafanikio huanza dharau,kiburi majivuno na kusahau kwamba unyenyekevu ndio ulimweka pale juu na juhuhudi.Mara nyingine hupoteza juhudi za mwanzo alizokuwa nazo na kuanza kulewa na kuwango kidogo cha mafanikio.Ni muhimu unapopanda kuelekea kiwango cha juu cha mafanikio hausahau ujenzi wa tabaia njema kila wakati ,Maana kama tabia njema inaweza kukuweka juu ,basi tabia hiyo hiyo inaweza kukushusha chini. Tabia Njema Ina Ujira na Malipo Mema Zaidi.Kila jambo mwanadamu alifanyalo lina malipo yake na faidia zake.Unapokosa tabia njema maana yake tabia yako ni mbaya basi tarajia matokeo yale yatokanayo na ubaya wa tabaia yako.Usisalalamike kwa malipo unayoyapata maana ndilo fungu ulilolichagua.Iwapo unataka ujira mwema kwenye maisha yako hakikisha unajenga tabaia njema.Usalamumu wengine sababu ya malipo mabaya unayoyapata leo,chunguza aina ya tabia uliyo nayo . Aina ya watu ulio nao kwenye maisha yako wanaweza kutuambia aina ya tabia ulio nayo.Ni muhimu pia kutambua hatua muhimu za ujenzi wa tabia yako unao taka kuufanya.Hakikisha Unajenga tabia njema ili upate Ujira mwema na wenye faida katika siku zako za uhai hapa ulimwenguni. Mwisho ,Hata Mungu kabla hajakubarikia huangalia aina ya tabia ulio nayo kuelekea mafanikio ambayo atakubarikia.Mungu haangalii kipaji chako zaidi ya tabia yako,Mungu huangalia tabia yako zaidi ya Kipaji chako.Watu wengi wenye vipaji hawanufaiki na vipaji vyao sababu ya tabia zao na hata mafanikio yao yakija huwa na muda tu maana waliwekeza muda mrefu kwenye kujenga mafanikio yao huku wakisahau kinachobeba mafanikio ni tabia na sio fedha.Fedha ni ya muda tu lakini tabia yako ni jambo linalodumu ,Mafanikio yanweza kuja na kuondoka lakini tabia yako ni swala ambalo lipo tu.Ni muhimu kufahamu nguvu ya tabia ulio nayo kwenye maisha yako ya kila siku.Tabia Njema ni Mtaji wa Mambo Mengi lakini Tabia Mbaya ni Kifo cha Mambo Mengi kwenye maisha ya mwanadamu.

Email :naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless You All
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.