SOMO: ROHO WA UWEZA - MTUME MWINGIRA

Mtume Josephat Mwingira wa huduma ya Efatha Mwenge jijini Dar es salaam.

ROHO WA UWEZA
Ndiye Roho atendaye furaha katika maisha yetu, mtu wa Mungu lazima awe na nguvu ya Mungu. (Zakaria.6:1). Ukisoma kitabu cha Zakaria, kulikuwa na farasi weusi, wekundu, weupe na wakijivu, kupitia hao farasi wanne tunajifunza kuwa kuna makundi manne yatuonyeshayo uwezo wa Mungu. Kulikuwa pia na magari ya vita manne, yenye farasi weusi,  weupe, wekundu, na wakijivu, walioenda Mashariki, Kaskazini Kusini na Duniani kote. Wale walioenda kaskazini walituliza moyo wa Mungu, magari hayo yalikuwa yanatoka katika vilima viwili.
Tusome Efeso 3:4, katika kitabu hiki tunaona magari yalitoka mbele za Mungu na kwenda duniani kote.
Pia tunajifunza kuwa kulikuwa na milima na Milima hiyo ni milima ya shaba. Tunajifunza mashuleni kuwa shaba haivunjiki bali hujikunja kwahiyo kama watu wa Mungu tunatakiwa kuwa kama shaba ambao iko imara na haikubali kuvunjika hata kama inapita katika misukosuko. Biblia inatupa mwangaza na ndio maana Agano la kale na Agano jipya litatudumu milele na lilikuwa likilenga maswala ya kitume na kinabii, kwahiyo Biblia ni nguzo la muhimili wetu wa Kikristo. Tunahitaji kusoma Neno la Mungu na kusoma vitabu mbalimbali kwaajili ya kujua mambo mengi ya Mungu.
TUONE MAANA ZA HAWA FARASI WANAOZUNGUMZIWA KATIKA KITABU CHA ZAKARIA
FARASI WEKUNDU: Farasi hawa wanazungumnzia ukombozi, damu itakayo kuokoa na kukutakasa.
FARASI WEUPE: Maana yake ni utakatifu
FARASI WEUSI: Maana yake ni uovu
FARASI WA KIJIVU: Maana yake ni msumari aliyopigiwa Yesu Kristo msalabani.
Farasi wanne wanabeba ujumbe mzima wa kile kilichotendeka, farasi wanne hao ni pepo wanne wa mbinguni.

TUONE MAANA YA PANDE NNE ZILIZOZUNGUMZIWA KATIKA KITABU CHA ZAKARIA
Upande wa kaskazini: Maana yake ni moyo wa mwanadamu. Yesu alibeba uovu wetu na kwenda nao msalabani ili kila amwaminiye asipotee ili apate wokovu na ndio maana tunaona farasi weupe wanamfuata. Yesu alibeba maovu yetu na akafa msalabani. Upande huu unaleta maajabu mengi sana.
Upande wa kusini: (Farasi wa kijivu). Yesu alisulubiwa kusini mwa Yerusalemu, na baada ya hapo wakampigilia msalabani. Na hayo yote Yesu alikubali ili wewe na mimi tupate kuokolewa. Huu ni upenda wa ajabu sana, hakuna mwanadamu aliyewahi kufanya haya yote aliyofanya Yesu ya kukubali kusulubiwa kwaajili ya kuokoa mioyo ya watu. Lengo zima la kuteseka ni kukuweka wewe huru na kufurahia maisha yako ya duniani na siku ile ya kufa kwako ukafurahie maisha ya mbinguni.
Dunia yote: Tendo la kumwaga damu lilisababisha dunia kumpenda Kristo, na sisi tukasamehewa maovu yetu, ka kupigwa kwake sisi tumeokolewa. Hapa ndipo ilipo nguvu ya Neno la Mungu. Tusome Ezekieli 47: Tunashuhudia sasa kuwa Yesu Kristo anajulikana duniani kote iwe mijini au vijijini jina la Yesu limetapakaa na kutamkwa vinywani mwa watu. Hata kama kuna watu wanampiga huyu Bwana Yesu lakini bado wanatambua kuwa kuna mtumishi wa Mungu aliweza kukubali kufa na hatimaye kufuka ambaye ni Yesu Kristo.
Upande wa Mashariki: Maji yaliyotokea ubavuni mwa Yesu na hayo maji mtu  anayesogelea anapata uponyaji. Na ndio maana mtu akiombewa Mungu anafanya uponyaji ndani ya mtu Yule amabaye naumwa. Kwahiyo maji ni uzima wetu.
Roho wa Uweza ni lugha ya mafumbo na huyo Roho wa Uweza amejificha sana, na kumtafuta inahitaji mtu aliyempenda Mungu, na kufanya kwa bidii kumtafuta Mungu. Tunaweza kufananisha na pesa, unapokuwa na pesa unaificha sana mfukoni mwako au ndani ya nyumba yako kwasababu kuipata fedha kunahitaji akili nyingi na juhudi zako.
MAMBO YANATOWEZA KUTOKEA BAADA YA KUPOKEA WOKOVU
Ukisoma kitabu cha Yohana 1:12, ulipokubali kumpokea Kristo na kufanya toba na kusema Yesu utamtumikia, unakuwa farasi wa Yesu na  yeye anakupenda. (Mathayo 11), Bwana anasema jitie nira, kwa hiyo farasi ukimtia nira maana unataka kumpanda na kumuongoza unakotaka kwenda. Na sisi tumefanyika farasi wa Yesu na dio maana tunaongozwa na Yeye na anatulisha na kutufisha kama vile farasi akishatumika anahitaji kula na kuvaa kwasababu ametii na amefanya kile ulichokuwa unataka afanye.
Roho ya uweza inafanya maajabu kwa mtu, wokovu ni Roho ambayo inatembea katika Roho wa uweza, na husababisha watu kuitwa wana wa Mungu.

Ukisoma katika kitabu cha Luka 6:19, Roho wa Uweza anapoingia ndani ya mtu unamfanya kuwa mtoto wa Mungu. Roho wa uweza amegawanyika katika makundi manne ambayo ni Toba, Maombi, Maji na  unafikia wakati wa kuchambua neno na kuhubiria watu.

Roho wa uwezo (Wafilipi 4:13): Uukifika hatua hii anakuwezesha kufanya mambo yote. Wewe mwanamke kama kuna wakaka walikuwa wanakukataa na kukukimbia, sasa utaona wakaka wanajikanyaga wakitaka kukuoa. Kumbuka mwanamke ni zawadi na ndio maana mwanaume anakaa na kuomba mwanamke wa kumuoa.

Mungu anaangalia wokovu wako, kwasababu Roho ya uweza ipo ndani yako, usivuke nafasi ya Mungu kwa kufanya mambo yako bila ya kumtanguliza Mungu. Mungu anasema pasipo yeye hakuna lililofanyika.

Roho wa Uweza kwa mtu wake anamsababisha mtu wa kuwa wa aina Fulani, wanawake wengi wanalia kuwa Mungu amewasahau bure na hiyo sio kweli. Wakumbuke kuwa wanahitaji kuwa na Roho wa Uweza ndani yao ili aweze kufungua milango iliyofungwa na maadui zao.

Kila mtu anatakiwa kuwa na kitu Fulani ndani yake ambacho kinafanya mtu afurahi. Ukiwa na Roho wa uweza ndani yako anakuganga mwenyewe na kufanya miujiza. Unaweza ukashangaa unaomba na watu wanapokea miujiza yao kwasababu Mungu amekukubali na umekuwa na kibali mbele za watu, kila jambo ukifanya linapokelewa na kukubalika na jamii.

Ukisoma katika kitabu cha Zaburi 34:7, Malaika wa Bwana ni Roho wa Uweza – ambaye ni muhimu maishani mwetu, na huangalia wamchao Bwana kwanza ili kufanya maajabu yake. Mungu hubariki Yule amchae. Jitahidi kupende kuwa na Roho wa ibada  ndani yako na kusababisha uweza utoke ndani yako. Kama ni mfanya biashara utaona wateja wanamiminika kwasababu Mungu amekukubali
Mungu akiona ibada ipo ndani yako anafanya makao ndani yako na hapo utaona mabadiliko katika maisha yako. Sasa unatakiwa kuona njia zako na sio matendo.

Inawezekana kufanya mambo yasiyowezekana kama unakubali kuacha dhambi na kumkubali Yesu. Uwe na mawazo ya kuwaza baadae yako na pia uwe mwombaji mambo yako ya ubaadae wako na kwa kuwaleta watu kwa Yesu.

VITU VYA KUFANYA ILI KUFANYA YASIYOWEZEKANA YAWEZEKANE:
i.                 Ishi maisha matakatifu
ii.                Uwe mtu wa maombi
iii.               Walete watu kwa Yesu
iv.               Mungu anaruhusu maajabu yake

JITAHIDI KUWA MTU WA IBADA ILI YAFUATAYO YATOKEE:
I.                 Tabia ya mawazo ya dhambi inatoweka
II.                Roho wa ibada anaumbika kwako
III.               Roho wa uweza anakuwa ndani yako
Roho wa uweza anakupa wewe ujasiri, maana hakuna kitu kitakacho kushinda na kusababisha kufikia mahali ambapo unataka kufika. Ondoa uvivu, uongo, umbea bali tamani kumjua Mungu, Mungu anakubali wale waliokubalika.

Somo limeandaliwa na RUMAFRICA
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.