SOMO: SABABU TANO ZA KWANINI MUNGU ANAINUA MTOTO/KIJANA - MWALIMU MWAKASEGESOMO: SABABU TANO ZA KWANINI MUNGU ANAINUA MTOTO/KIJANA KWA AJILI YA UTUMISHI WAKE WAKATI WATU WAZIMA WAPO

Pata dondoo za somo hili kama lilivyofundishwa na Mwalimu Christopher Mwakasege jumapili iliyopita wakati wa semina ya vijana iliyofanyika katika usharika wa Kilutheri wa Mbezi Beach jijini Dar es salaam.


1. Ndio muda ambao watu wazima wanafunga maagano na MUNGU.

2. Ni wakati mahusiano ya watu wazima na MUNGU yanapoa, yakipoa MUNGU anatafuta mtoto/kijana achukue utumishi.

👇1 Samweli 3:1~10
Samweli aliitwa akiwa mtoto mdogo,kipindi ambacho neno la BWANA lilikuwa adimu. Aliitwa kipindi ambacho hata hakuwa anajua sauti ya BWANA.

MUNGU alijifunua kwa Samweli akiwa bado mtoto.

3. Ni wakati watu wazimu wanapomdharau MUNGU wao wanapojikuta wamesongwa na matatizo katika maisha yao.

👇Hesabu 13
Maagizo ya MUNGU juu ya Musa kuhusu kwenda kupeleleza Kanani, na walete taarifa na kisha walete na matunda. Walipewa kufanya utafiti wa awali juu ya nchi(ardhi,mipaka) na watu. Watazame ndani kama watu ni wachache au wengi, nchi ya unono au njaa . Wakate matunda na waende nao ili ijulikane walitengeneza takwimu au walifika mpk Kanani. Iliwachukua siku 40.

👇Hesabu 13:30
Hawakupewa kutafiti nafsi ila wao walifanya hivo.

👇Hesabu 14:11.26~31
9 Joshua na Kalabu walikuja na mtazamo tofauti,na wenzao wakataka kuwapiga mawe ,ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana kwenye hema.

Musa na Kalebu walishindwa kuingia Kanani kwa sababu walishindwa kumuamini MUNGU.
MUNGU aliwatuma kupeleleza ili wajue cha kufanya kwa vile ambavyo watakavyoikuta. Musa na Kalebu walishindwa kutafsiri picha wanayoiona katika sura ya KIMUNGU ndo maana. Walishindwa kuiona vision katika tatizo lile.

Mtu anayeogopa matatizo ameogopa maono. Kama ulimuona MUNGU kwenye matatizo jana, juzi,kwanini unashindwa kuona atakusaidia kwenye tatizo lako la leo?? Acha kumdharau MUNGU.

Fikra zako lazima zichanganywe na uwepo wa MUNGU ili kuweza kutatua tatizo ulilo nalo.

MUNGU anapoona watu wazima wanalalamika juu ya matatizo yaliyopo yamekwama, ananyanyua watoto/vijana ili wabadilishe mazingira yaliyopo katika jamii ile.

MUNGU anampa mtoto/kijana macho ya kuona jinsi ya kutatua tatizo lilolowashinda watu wazima.

4. Kwa sababu ya utumishi wa kurithi kifo kinapotokea.

👇2 Wafalme 14:17~21
    2 Wafalme 15:1~2 "Mfalme alitawala akiwa na miaka 16 na alitawala kwa miaka 50"
MUNGU anaweza kumgusa mtu akiwa mdogo ili aweke hifadhi ya ile mbegu mapema ili kitunzwe na kisifukuzwe.

👇Waebrania 9:16~17
Utumishi wa MUNGU ni wa kurithi

Kuna kurithi kwa aina 2
1. Kuna urithi ambao ukiwa ndani ya MUNGU unapewa. Ilikuwa lazima YESU afe ili utumishi uwe na nguvu.

2. Liko agano la kurithi ambalo liko kwenye familia,familia ya kanisa, biashara,uongozi na nk

Agano la urithi lazima iwepo mauti. Mfano Musa alipokufa  MUNGU alikuwa amemuandaa  Joshua ili arithi agano la uongozi,ili kutekeleza kusudi la MUNGU.

If u don't prepare,you won't occupy.

5. Kwa ajili ya kutunza ushuhuda kwa utukufu wa MUNGU katika kizazi na eneo

👇Zaburi 37:25
*Wenye haki na wasio haki wanavyoishi
*Mwenye haki haachwi tangu ujana mpk uzee
*MUNGU alimgusa Daudi akiwa kijana na akaenda nae mpk uzee
*MUNGU hufanya kazi na wale wanaosimama kwenye kusudi lake hata kama uliwahi mtenda dhambi (Mfano wa Daudi) maana atatengeneza na wewe maana yeye yupo.
* Daudi hakuwa perfect ila alikuwa karibu na MUNGU sana
* MUNGU anataka akuguse ukiwaa kijana ili ushuhuda wako uwepo mpaka ukiwa mzee

Kama upo shule, kazini, kwenye biashara na MUNGU anakuita kwenye utumishi wake, usiache bali muulize hapo hapo ulipo utatumika vipi?
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.