SOMO: UMECHAGULIWA KWA WALIO WAKO

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.Moja ya changamoto tunayokabiliana na kizazi hiki ni kutambua wapi umechaguliwa na wapi haujachaguliwa na kwa nini hapa umechaguliwa na pale haujachaguliwa na unapaswa ufanye nini unapogundua kuna mahali umechaguliwa na mahali ambapo haujachaguliwa.

Hakuna mtu ambaye amechaguliwa kutumika kwa kila mtu kwenye maisha yetu haya ya kila siku.Ni Muhimu kutambua kwamba kuna maeneo kwenye maisha yako unaweza kukubalika na kuna maeneo hauwezi kukubalika. Maisha yako na namna ulivyoumbwa ni dhahiri ya kwamba kuna eneo la watu  umechaguliwa uwatumikie.Huku ulimwenguni hautakubalika na kila mtu na hautapingwa na kila mtu ni muhimu kufahamu wapi unakubalika na wapi haukabali na baada ya kufahamu  nini cha kufanya baada ya kufahamu hilo.

Mara nyingi huwa watu wengi tunalazimisha  kukubalika na kila mtu na kila mahali na kila tunachofanya wakati ni ngumu.Tambua hauwezi kukubalika na kila mtu na hauwezi kupendwa na kila mtu.Kuna wengine watakuambia,Kuna wengine wakuangalia tu. Kuna wengine hawakuambia lakini ndani ya mioyo yao hawakukubali.Kutokukubali kwao sio dalili ya uadui au ubaya ni namna tulivyouumbwa tofauti.Hauwezi kukuta vidole vya miguu vinafwanana na vidole vya mikono ingawa vyote ni vidole.Ni muhimu kujifunza na kutambua hivyo ,hii itakusaidia kukupunguzi misongo ya mawazo isiyokuwa na ulazima.

Tambua  Eneo Unalokubalika ndio eneo lako la kukua na kustawi,Hakikisha unatumia muda mwingi kulipalilia na kulikuza eneo ambalo unafahamu unakubalika.Acha kupoteza muda mwingi kujaribu kuwashawishi watu ambao hawakukubali ,tambua haujaitwa kwao.Eneo unalokubalika ni mithili ya udongo mzuri unaoweza kupanda mbegu na ikastawi.Eneo usilokubalika ni mithili ya eneo ambalo limesongwa na  miiba hata ukipanda mbegu si rahisi kumea kwa urahisi.Tumia muda mwingi kujiimairisha eneo unalokubalika maana ndio mtaji muhimu kwa ajili ya maisha yako.

Eneo Unalokubalika ni eneo linaloweza kuamua hatma ya maisha yako ya siku zijazo.Pale unapoona unakubalika ni ishara unaweza kustawi na maamuzi yako mengi yanaweza kuamuliwa na namna unavyokubalika kwenye eneo hilo. Haimaanishi uwadharau watu ambao hawakukubali bali lazima ujifunze kuweka vipa umbele kwenye eneo la kibali. Pote ulipochaguliwa kibali huwa kinatangulia mbele yako. Epuka kutumia nguvu kupata kibali au kubalika kwenye eneo husika.Acha watu/jamii ikuridhie yenyewe ndipo unaweza ukaona matunda siku zako za mbeleni.Mahali popote usipokubalika utakuwa na wakati mgumu katika kustawi kwako kwenye siku zijazo.Unaweza kustawi lakini hautastawi katika kiwango kile unachofikiria unapaswa kustawi.

Usijenge hoja na mtazamo wa chuki kwa watu ambao unaona hawakukubali tambua kwamba wao wana watu wao wanapata kibali kwenye mioyo yao ni muhimu kutambua hilo. Lakini pia tambua kipindi tunaishi hapa ulimwenguni hakuna mtu anayeza kuwa na adui wa kudumu maana unaemuona hakukubali leo anaweza kukubali kesho na unamuona anakukubali leo kwenye eneo fulani anaweza asikukubali kesho.Ni muhimu kuhakikisha unaishi kwa amani na kila mmoja maana hakuna anayeweza kuijua kesho yake inafwanana namna gani.

Jifunze kutuumia Muda wako vyema kujiimarisha kwa watu ambao unakubalika kwao maana ndio eneo la kutumika kwako.Tumika hapo kabla ya kufikiria kwenda eneo ambalo unaona haukubaliki.Mara nyingi sheria za asili huwapa nafasi wale ambao hujua namna ya kuzitumia na kuzifwata kwa usahihi.Sheria ya Asili Moja Wapo ,Inaitwa Sheria ya Kibali. Sheria ya Kibali haipendelei maana ipo tu ,Sheria ya Kibali hutoa kibali kwa kwa kila moja kutoka na namna alivyoumbwa.Huwezi kukuta jicho linalazimicha litumike kwenye mguu na mguu utumike kama mdomo.Mguu hutumia eneo lake la asili uliopewa kibali kuwepo lakini pia Mguu haupingi jicho kwa sababu jicho halimkubali Mguu alipo,Viungo vyote huungana na kufanya kazi kwa pamoja.Ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kila siku na kwenye utumishi ambao tulio nao hapa ulimwenguni.

Mwisho  Ukitaka kujua tabia ya mtu alivyo nafsi mwake,chunguza watu anao wapenda na anao wakubali.Unaweza kukuta haupati kibali sehemu si kwamba una tatizo bali ni namna ya watu waliokuzunguka.Watu Ambao watu wengine wanawakubali na wanapenda wana ushawishi mkubwa sana kwenye tabia zao za asili.Usizalimishe kukubalika sehemu maana unaweza ukaukuta unashawishiwa kubadili tabia yako njema ulio nayo.Jifunze kutafuta walio wa kaliba yako na utumike kwao bila kinyongo na bila kutumia Nguvu.


E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.