SOMO: TAARIFA MBAYA IKIFANYIWA KAZI HUZAA TAARIFA NZURI

Mchungaji Gasper Madumla.

Bwana Yesu asifiwe…
Usipende saana kuambiwa taharifa nzuri kila siku maana hutaweza kuzifanyia kazi ipasavyo taharifa hizo,bali penda pia kupewa taharifa mbaya juu yako ambazo zitakusukuma kuzifanyia kazi.Piaufahamu yule akuambiaye siku zote taharifa nzuri nzuri tu pasipo kukwambia na mabaya,basi ujue si rafiki mzuri sana,tena yawezekana hana lengo la wewe kukua vizuri kiroho. Mfano pata picha rafiki yako anakuambia kila siku kwamba ” …upo vizuri wewe huna chochote kibaya,… ” Kisha fikiria tena upande wa pili wa rafiki akuambiaye ” Nimeona roho ya magonjwa juu yako,tena ipo roho ya uchawi inakufuatilia...” Kwa mifano hiyo miwili waweza kujua ni jinsi gani wapi utakuwa na msukumo wa kuomba kwa sababu ya taharifa hizo.
Watu wengi hupenda kuambiwa mazuri tu,lakini kuambiwa mabaya hawataki. Sasa hii sio staili ya mkristo aliye hai,maana mkristo aliye hai hukubali kuambiwa yote yote mabaya na mazuri,tena hasa mabaya ili kupitia hayo azidi kuongeza kasi ya kumtafuta Mungu wa kweli.
Sikia hii;
Siku moja nilimualika mtumishi wa Mungu mwimbaji wa nyimbo za injili,alipomaliza kuhudumu-kesho yake akanipigia simu na kuniambia mambo aliyosukumwa na Mungu aniambie,~of coursetaharifa aliyokuwa akinipa haikuwa nzuri hata kidogo na akaniomba kwamba ikiwezekana mimi na wachungaji wenzangu tufunge na kuomba kuzuia yale yote aliyokuwa akiyaona katika taharifa ile.Hiviunajua nami nikawaambia wachungaji wenzangu tuingie katika mfungo na maombi ya kina,na hatimaye mambo mengi yalifunguka.
Sasa unisikilize,kama mtoa taharifa asingeniambia eti kwa sababu ya taharifa kuwa mbaya,hivi unafikiri tungeliweza kuingia katika mfungo na maombi?.Ok chukulia hata kama taharifa ile niliyopewa haikuwa na uhalisia kwa kile alichokua anakiona,kwamba chukulia kama ametunga vile,Lakini kumbuka hata kama ingelikuwa hivyo ya kutungwa lakini bado sisi tumeifanyia kazi na kuleta matunda katika kanisa. Laiti angelitupea habari njema tu,tusingelikuwa na kiu kubwa ya kufunga na kuomba.Hivyo taharifa mbaya tuliyoipokea ikazaa matokeo yenye taharifa nzuri.
Biblia inasema;
” Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliopona, hao watu wa uhamisho waliosalia; na habari za Yerusalemu.
Wakaniambia, Watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni; Nehemia 1:2-4
Nehemia anatueleza namna alivyopewa taharifa mbaya ya masikitiko iliyompelekea alie siku kadha wa kadha na afunge pamoja na maombi,na baada ya maombi hayo tunaona majibu mazuri yakipatikana. Baada ya kufanyiwa kazi taharifa hizo mbaya zilizoletwa na Hanania mmoja wa ndugu wa Nehemia,tunaona sasa taharifa hizo zinabadilika na kuwa taharifa nzuri,ndio maana nami nakuambia kwamba taharifa yoyote ile mbaya,ikifanyiwa kazi huwa ni taharifa nzuri kwa utukufu wa Bwana. Ingelikuwa ni vigumu kwa Nehemia kulia,kufunga na kuomba kwa mzigo laiti kama asingelipewa taharifa mbaya juu ya ndugu zake.
Kumbuka;
Mtu anaweza kuwa amekutungia habari moja mbaya sana juu yako kwa lengo la kukuchafua au kukualibia sifa yako.Hata kama hali itakuwa ni hivyo basi wewe penda kuisikiza mpaka mwisho wala usimkatishe kama akiwa anakuambia then fanyia kazi taharifa hizo kwa hekima. Ninajua kwamba wapo watu wenyekuzusha mambo ya uongo,yajapo mambo kama hayo wewe usiumize kichwa sana kwa kuyafuatilia maana utakuja kupoteza muda wako bure! Bali wewe songa mbele katika maisha yako ya wokovu.
Kwa huduma ya maombi na maombezi usisite kunipigia simu yangu;0655 111149
Mch.Gasper Madumla.
Beroya bible fellowship church. (Dar-Tanzania)
UBARIKIWE.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.