WACHAWI MKOANI LINDI WATUMA MKIA WA FARASI MKUTANONI KUMDONDOSHA MHUBIRI

Hapana shaka bado unakumbuka shuhuda ambazo tumewahi kukuandikia humu kuhusiana na jinsi Mungu anavyoitumia huduma ya VHM iliyochini ya mchungaji Peter Mitimingi kuharibu kazi za shetani na mawakala wake wanaotesa watu kwa vitendo vya kishirikina hasa sehemu ambazo hazijafikiwa na injili. Leo ni ushuhuda mwingine kutoka katika huduma hiyo ambayo ilipiga kambi mkoani Lindi ili kumtangaza Kristo kwa wakazi wa mkoa huo, ambapo Yesu alijidhihirisha kwa kutenda mambo makuu. Soma ushuhuda chini kama ulivyoelezewa na mkurugenzi wa huduma hiyo mchungaji Peter Mitimingi.

Mkia uliotumwa na wachawi ukiwa umejikita aridhini
WACHAWI WAUTUMA MKIA WA FARASI MKUTANONI KUMDODONSHA MHUBIRI!
Ni ajabu na kweli. Wachawi wa hapa Lindi baada ya kujaribu kutuloga kwa njia mbalimbali na kushindikana walituma mkia wa farasi ukiwa umefungwa kitambaa chekundu. Mkia huyo haukurushwa bali ukikuwa ukielea kutoka angani mpaka ukafika kwenye eneo la mkutano na kujichomeka wenyewe aridhini na kusimama. Tukio hilo liliwashangaza sana watu wote waliokuwa wamaketi chini kusikiliza neno la Mungu.

Baada ya kudondoka kwa mkia huo watu wengi waliokuwa wamekuja kusikia injili walikimbia na kusimama mbali mpaka makomandoo wa VHM waliposogelea na kuushika mkia. Mkia wa farasi ulidondoka kutoka juu kwenye uwanja wa mkutano huko vijiji vya lindi. Ulitumwa na wachawi kama kombora la kusambaratisha jeshi la Bwana.
Tulichukua mafuta ya taa na kuuchoma moto chakushangaza mkia huo ulikuwa unagoma kuungua yaani moto unawaka lakini mkia hauungui. Ndipo tulipoleta mafuta ya Petrol na kumwagia kisha kuuchoma kwa petrol huku tukiomba na moto wa Yesu ndio taratibu mkia huo ukaanza kuungua.Wakati tukiwa tunauchoma mkia huo kwa moto wa petrol huku tukiimba na kuomba moto na damu ya Yesu ghafla tulishangaa kuona vinyoka vingi vikitoka katika ule mkia wa farasi uliokuwa ukiungua moto. Na chakushangaza zaidi ni pale ambapo vinyoka hivyo vilikuwa vikitembea ndani ya moto bila kuungua kwa muda mpaka tulipoongezea petrol na kuongeza maombi vikaanza kukimbia moto ndipo tulipochukua jembe na kuanza kuvikata kwa jembe na kuvirudishia kwenye moto na baadaye viliungua na mkia wenyewe na kufa.
Yesu anatenda makuu huku vijiji vya Lindi.

 YESU AMEFANYA MAMBO MAKUBWA SANA VIJIJI VYA LINDI!

 


Huduma ya VHM imekuwa ikijishughulisha na injili sehemu za vijijini na mijini ambako kuna ugumu wa injili kufikika kwa urahisi hasa kutokana na sifa za kuwepo nguvu za kishirikina ama kutowahi kusikika injili kabisa na watu wamekuwa wakionewa na nguvu za giza. Ili kujua mengi kuhusu huduma hii ama kutaka kuchangia huduma hii ofisi zao zipo Mwenge jijini Dar es salaam karibu na hospitali ya mama Ngoma au wapigie simu ifuatayo 0713 183 939

Kusoma shuhuda nyingine kutoka VHM BONYEZA HAPA
                                                                       
                                                                      BONYEZA HAPA


                                                                       BONYEZA HAPA
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.